Na Msalaba Benard
Nipo naendelea kutafakari ushiriki wa timu zetu kunako michuano mbalimbali.
Nipo najaribu kubainisha ni mambo gani yanatutesa hata hatufiki mbali.
Kuna mengi mengine mtayasema wadau ila kwa upande wangu ningependa kudodosa hili la mechi za ugenini.
Nimebaini mara kadhaa tunafanya vema hapa nyumbani ila tunateseka ugenini.
si tu kwa idadi tu ya goli tunazofungwa bali pia 'Performance' yetu (viwango vya timu zetu vikiwa ugenini)
Mbaya zaidi nimebaini hatutumii vema mechi za nyumbani na wakati mwingine tunapumbazwa na wageni wetu.
Tutawashambulia tunakosa nafasi za wazi, tutapata ushindi mwembamba ama sare kisha tutajifariji kungoja miujiza ugenini.
Ona, Mara chache wageni watafunguka wanapocheza hapa. Watatushambulia mara moja moja hususani wakishafungwa.
Ona, Mara chache wageni watacheza kwa kasi. Muda mwingi watajiangusha na kulalama na mwamuzi. Kumbe wanatuzuga.
Ona, Mara chache watatuonesha uwezo wao ambao sio halisi ila huo mtiti wa mechi za ugenini si wa kawaida.
Ona, Watatukimbiza na kutushambulia, wale wale ila hawatoanguka anguka, muda wote wataonesha kiu ya kutufunga.
Kuna mdau kanambia Yanga hawawezi waarabu labda angekuwa Simba nimemkatalia.
Nimemwambia ni sawa nakubali Simba hujitahidi ila bado anateseka mechi za ugenini, hususani zile zile dhidi ya timu za kaskazini.
Nimemsisitizia Si Simba, si Yanga, si Azam si Taifa Stars mechi za ugenini zinatutesa.
Ona, Ni mechi chache utasifia 'performances' yetu ugenini.
Tizama, Mara nyingi zote zitafungwa na wakisharejea tutasikia wakilia fitina na figisu.
Binafsi, kwa miaka 10 ilopita performance bora zaidi kwa timu zetu Uarabuni ni ile ya Yanga na Al Ahly 2015.
Japo walitolewa lakini walicheza na wadau wao wakaridhika na kusuuzika mioyo Yao.
Kuna mdau kanambia hukuiona Simba ilipomnyoa Es Setif? Nimemkumbusha Simba waliteseka sana siku ile.
Nimekumbusha kilichoisaidia simba iliingia Algeria na faida ya goli 2 kisha wakangoja jaribio la Emmanuel Okwi lililozaa faida ya goli la ugenini dk za majeruhi.
Nimekumbusha pia 2012 Simba alimfunga Al Shendy 3-0 hapa akafa 3-0 tena dk 45 za pili za ugenini kisha akatolewa kwa penati.
Nimekumbusha 2011, Simba alimvua Ubingwa wa Afrika TP Mazembe kwa kanuni akapangwa na Wydad Casablanca akapigwa 3-0. Goli zote zikifungwa dk 5 za mwisho.
Nimekumbusha tena mnamo 2009, Simba alimnyoa Harras El Hadood 2-0 taifa, akaenda akanyongwa 5-1 Ugenini.
Anyway niseme tu si lengo la kijimakala hiki kulinganisha rekodi za Yanga na Simba bali nakusudia tutafakari namna vilabu vyetu vinavyojiandaa na kuzikabili za ugenini. Hususani zile za kasikazini.
Kwenu benchi la ufundi na viongozi Nanyi mjue ni wakati wa kuwa na mipango thabiti. timu zetu ziandaeni kikamilifu.
Msisite hata kuomba ushauri kwa wale waloshiriki tulipofanya vizuri huko Uarabuni.
Jipangeni amueni tukijizatiti tunaweza. Ni nani hakumbuki Simba ilisimama kidété ikawatoa Zamalek kwao 2003?
Ni nani kasahau Yanga nusura amuumbue Al Ahly msimu Ulopita?
Ni nani hakumbuki Yanga ilivyokaza mpaka kutolewa kwa matuta na Al Ahly 2014?
Ama ni nani hakumbuki Yanga hiyo hiyo ilivyojaribia kuiduwaza Étoile du sahel 2015?
Anyway, tusiishie kuwa watu wa kumbukumbu. Tuamue, tufanye kweli. Naomba kuwasilisha.
No comments:
Post a Comment