RASHFORD JIFICHE, KAMERA ISIKUMULIKE.
Ninacheeeka sana, nina furaha na amani moyoni, sio kwa ajili ya ushindi wa Man U dhidi ya Arsenal, nimekumbuka enzi zangu za utoto. Miaka takribani 15-19 iliyopita, nilikuwa mtoto, mtoto wa maajabu naweza kujiita. Nadhani ndio nililelewa hivyo na wazazi wangu, kuwa kila kitu ninachoona nikakipenda basi ninaweza kukifanya, tena kwa ufanisi. Nilikuwa nina juhudi ya kujua kila kilicho bora. Ilikuwa sio ajabu ukinikuta ninawasimulia watoto wenzangu habari za siasa za magharibi kipindi cha vita baridi, wala haikushangaza kunikuta nikiwafundisha hata watoto wa kiisalamu habari za Yesu kristo, sasa habari ya mpira na kuwajua wachezaji wa ulaya nadhani mtaani kwetu na hata shuleni nilikuwa na wapinzani wachache sana ambao mpaka leo nawakumbuka kwa majina. Lakini pamoja na ujuvi huu nilikuwa siwezi kuishinda aibu na uoga. Nilikuwa najificha mbele ya wageni na hata inaponilazimu kukaa mbele yao nilikuwa mkimya sana. Baba yangu, wakati huo, alinipenda na akanitumia vzuri kama nishani ya kung'aza sifa za familia. "Aah ka kijana kangu haka, ka G, kanajua wachezaji woote wa dunia nzima" ilikuwa kauli maarufu pale stori zinapopamba moto baina ya mzee na marafiki zake, wakati mwingine " ka G kanatengeneza vifaa vya umeme, iwe TV, rimoti hata pasi". Nilijisikia fahari sana, ila mshangao mara nyingi ulizikumba nyuso za wasimuliwaji. Hawakuweza kuoanisha kati ya udogo wangu na makubwa yanayonenwa, jambo ambalo lilinifanya kuwaduwaza pale ninapopewa nafasi ya kuthibitisha maneno ya baba. Nilikuwa katoto kapenda sifa ambako hakajioneshi, kanasubiri kuwaduwaza watu.
Jina ambalo limepata umaarufu wa ghafla kuanzia Carrington, AON complex mpaka Old trafford wiki hii ni, Marcus Rashford. Sio mengi sana tunaweza kuyajua kuhusu huyu kijana. Alizaliwa tarehe 31 mwezi wa 10 mwaka 1997 (anazidiana miezi miwili tu na mdogo wangu anayenifuata). Mtoto huyu alianza kucheza mechi yake ya kwanza kwenye kombe la FA la vijana dhidi ya Leicester mwaka 2014. Aliwashangaza walimu wake Paul McGuiness ambaye alisema ana kipaji cha aina yake na Warren Joyce ambaye aliamua kuanza kumtumia kama mshambuliaji wa mwisho katika kikosi cha vijana baada ya Mitchell kuumia na huyu dogo akaweza kuwa mfungaji bora wa msimu wa 2014/2015. Kwa mara ya kwanza ameingia uwanjani katika kikosi cha wakubwa kwenye mechi ya Europa dhidi ya Midtyjlland na kufunga goli mbili. Mshangao ni kuwa, alikuwa mtu wa mwisho kabisa kutajwa katika kikosi cha siku hiyo baada ya Anthony Martial kuumia mazoezini siku hiyo, lakini pamoja na hayo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga katika michuano ya ulaya. Jana dhidi ya Arsenal ameorodhesha jina lake kwenye orodha ya wachezaji wadogo waliowahi kuifungia United katika ligi kuu, yeye ni wa tatu baada ya Macheda na Welbeck. Nikimtazama Rashford, tangu katika mechi ya Europa ninaona washambuliaji fulani fulani ndani yake. Ninaweza kumuona Macheda ndani yake, ninamuona Berbatov ndani yake, na endapo atafanikiwa kuwa na msuli zaidi ya sasa anaweza kuwa Drogba. Sikupanga kumtilia maanani sana lakini vitendo vyake vya ujasiri mbele ya beki za Arsenal vimenivutia zaidi, kwa mtoto mdogo vile kuwa na ujasiri wa kutaka kukatiza katikati ya Bellerin na Paulista ama kutaka kukimbizana na Koscielny, ama kuweza kujiweka katika nafasi nzuri za kupokea krosi mbele ya ukuta wa Arsenal ni jambo la kustaajabisha. Hata hivyo ninakumbwa na wasi wasi kama alionao kocha wa Man U, Louis Van Gaal kwamba hawa vijana huweza kufanya vizuri mechi ya kwanza lakini suala ni mechi ya pili na ya tatu hadi ya nne na kuendelea, je, ataweza kuendeleza huu ubabe? Ataendelea kukua na kukomaa? Ni muda pekee ulioficha siri hii.
Kwa siku za karibuni, wameibuka vijana wenye vipaji vya aina yake. Wengine tukawafananisha na majina makubwa yaliyowahi kutokea katika soka. Tulitegemea makubwa kwao lakini wengine, tena wengi walituangusha. Wengi wamepotea. Wamekuwa wa kawaida sana na pengine wamekuwa wabovu. Inatunyima imani sana sasa kuwategemea sana watoto wadogo wenye kuonesha ishara nzuri. Moja ya vitu vinavyochangia sana hili ni vyombo vya habari. Vyombo vya habari viko macho sana kutafuta habari kuliko kuweka ukweli. Vinaishi kwa matukio kuliko uhalisia. Vyombo vya habari yaani magazeti, televisheni, redio na mitandao vinaweza kukufanya uishi maisha ambayo huyataki, vinaweza kukufanya ujaribu sana kuishi wanavyotaka na hapo ndio ugomvi wao na LVG, Mourinho na Ronaldo unapoanzia. Wanakuzonga, wanakukosesha raha. Lakini hili hunoga zaidi kwao unapoamua kuishi mbele ya kamera zao. Depay, Sterling, Januzaj, Walcott na wengine wengi ni wahanga sana wa suala hili. Utagundua kuwa hili tatizo liko uingereza sana. Anthony Martial amejificha, kamera zilimmulika mwanzoni lakini akajua jinsi ya kuishi nazo, hivi sasa hakuna ubishi kuwa Martial ni mchezaji muhimu Utd japokuwa hakustahili kuvaa majukumu hayo mapema hivi. Akina Messi na Neymar wamejifunza namna ya kuishi nyuma na sio mbele ya kamera, haziwasumbui tena. Ugonjwa bado uko uingereza.
Moyoni mwamgu natamani sana Rashford lije kuwa jina linalotamkwa sana huko baadae, natamani aje kuwa Van Nisterooy ama Rooney wa zamani yule ambaye mpaka sasa anaheshimiwa kwa matendo ya kale. Haya yanawezekana tu endapo atawekwa chini ya uangalizi wa watu wazima, asibebeshwe majukumu makubwa asiwekwe kila wakati. Ifike kipindi mashabiki wamtamani awepo na kila akiingia anatuachia cha kujadili mpaka atakaporudi. Ndio maana ninacheka, maana natamani Rashford awe kama 'ka G', mkimya, mwemye aibu mbele za watu, awe sifa mbele ya baba yake LVG, ili baba yake aweze kumtumia kama fimbo ya kuwaumiza adui zake. Cha kuchekesha ni kuwa Rashford hajawahi kuniona, na hajawahi kunisikia hata pengine wakati 'ka G' kanahangaika kung'arisha jina mbele ya wageni wa mzee yeye alikuwa ananyonya. Wakati huo nina ndoto za kuwa rubani na yeye hatambui kama ana mguu wa mpira. Lakini ni vyema sana akawa tu hivyo kama, itamjengea sana jina kubwa baadae. Ombi kwa meneja ni kwamba asimpange sana huyu dogo maana hata jeraha la Martial sio la muda mrefu. Rashford abaki kuwa "suprise package" hapaswi kabisa kuvipa mianya vyombo vya habari kuhangaika naye. Ni kweli anahitaji uzoefu zaidi, lakini huu ndio wakati ambao historia za akina Ronaldo, Messi, Xavi na Welbeck zinahitajika zaidi. Wengine pia ambao wanaweza kutumika kama "bad examples" wasisahaulike. Rashford ama Rashid kama anavyoitwa vibanda umiza anapaswa kuendelea kulelewa tu.
Wakati huu ni vigumu sana kwa Man u kuukubali ukweli huu maana watoto hawa ndio pekee waliopo. Na Timu inahitaji kushinda. Lakini kwa manufaa ya baadae mechi chache zijazo zinapaswa kumlea Rashford kuliko kumpa majukumu. Falsafa ya LVG inapenda sana kutengeneza vikosi vya baadae, lakini kwa maisha ya uingereza, sio vyema sana kuishi mbele ya vyombo vya habari. Uingereza na Tanzania ni kama tuna tamaduni zinafanana. Tunapenda kusema mambo kwa kuyakuza sana bila kujali athari zake kwa wasemwaji. Ndio maana huwa najivunia sana maisha ya 'ka G' maana kalipenda siku zote kuushangaza ulimwengu. Kukiweka katika namna ambayo hakuna mtu hutegemea kanachoweza kutenda. Ni kama tu kuishi nyuma ya mlango wakati unaujasiri wa kuonekana. Ningepata nafasi ya kuongea na mdogo wangu Marcus Rasford ningemsihi ajifiche, nyuma ya mlango, ili kamera za waingereza zisipate kummulika na kumfanya aishi maisha ambayo yeye hajayatamani. Nilifurahishwa na jibu lake, kwamba hatasherehekea ushindi maana leo ana mtihani wa Kemia, safi sana dogo. Hivyo hivyo, usiwe kama msanii wa bongo flava aina fulani fulani, ukitoa ngoma moja ikapigwa Kenya unanunua gari na kuanza starehe kisha unasahau kazi za studio. Piga kitabu, piga mpira, piga magoli lakini usisahau kabisa kuwa unapaswa ujifiche, kamera isikumulike.
~GULINJA E. GASPER~
IG & twitter :dc_gitaa