Wednesday, April 19, 2017

UTAWALA WA KIHASPANIOLA KATIKA SOKA LA ULAYA

WAHISPANIA WAMETAWALA SOKA LA ULAYA.WAKATI WA KUJIULIZA

Msimu uliopita Seville walitwaa ubingwa wa Ueropa league kwa kuifinga Liverpool 3-1 katika fainali.Ulikuwa ubingwa wa 3 mfululizo katika kipindi cha miaka 3 wakizifunga timu za Dinipro,Benfica na Liverpool.

Msimu huo huo 2015/2016 Real madrid walitwaa ubingwa wa ulaya kwa Mara ya 11 na Mara ya pili katika kipindi cha miaka 3.Fainali zote 2 wakiwafunga atletico madrid.

Nimekuwa kwa muda wa miaka 7 sasa nikifuatilia ubora wa ligi ya uhispania na ushiriki wao katika michuano ya ulaya.Wamekuwa wakitawala soka la ulaya kwrnye ligi ya mabingwa na ueropa.

Wahispania wameweza kuunda timu bora na za ushindani barani ulaya.Watazame Real madrid,Barcelona,Atletico madrid na Seville.

Mara nyingi wamekuwa wakionyesha upinzani mkubwa kwa vilabu toka uingereza,Ujeumani,Ufaransa na Italy.

Kwa Mfano klabu bora katika Bundesliga Bayern Munich imeshindwa kufulukuta mbele ya wahispaniola kwa mara ya nne mfululizo.Wamekuwa wakisumbuliwa na timu kutoka Spain.

Ukirudi katika kipindi cha miaka 3 timu kutoka Hispania zimefika fainali mara nyingi Kuliko klabu kutoka taifa lolote barani ulaya. Barcelona mara 1 (dhidi ya Juventus ) huku Real madrid sawa na atlerico madrid Mara 2.

Ubora wa vilabu hivyo upo kuanzia kwa wachezaji,Makocha na aina ya mbinu wanazotumia dhidi ya wapinzani.

Mpaka mda huu tayari Hispania wameishakata tiketi ya vilabu vya Atletico madrid na Real madrid kabla ya Mechi ya Barcelona na Juventus.

Ni dhahiri ukitaka ubingwa wa ulaya kwa sasa uweze kuvifunga vilabu vya Hispania   katika kila hatua unayoonana nao.

Huu ni wakati wa Mataifa kama Uingereza,ufaransa,ujerumani na Italy kufikilia kwanini hispania wanafanya vyema katika michuano ya ulaya.

Ligi ya Hispania imekuwa ikikosolewa kwa kukosa ushindani.Ushindani hauwezi kuwepo kutokana na Vilabu 3 kumiliki wachezaji wenye madaraja ya viwango vya dunia.

Hata bundesliga Bayern nao ndio ivyo,PSG na Juventus nao ndiyo ivyo ivyo.Huwezi kushindana na Timu hizo.

Kiufupi England wachezaji wanaviwango vinavyoshahibiana ndio maana unakuta kunakuwa kugumu.Matokeo yake ni kumanini kuwa wana timu bora kumbe sivyo.

UCHAMBUZI:REAL MADRID V BAYERN MUNICH

Na Timotheo John

MAMBO NILIYOYAONA REAL MADRID V BAYERN MUNICH

1.Bayern Munich hawana mpango B.
Katika mechi ya Kwanza Muller alianza huku lewandowiski akikaa nje kutokana na majeraha Jana Lewandowiski kaanza Huku Munich wakionekana kushambulia kwa kutumia mipira ya pembeni walifeli lakini hawakuweza kubadiki mbinu kwa kipindi cha kwanza na pili.

2.Ronaldo anafunga katika wakati sahihi
Katika hatua ya makundi Ronaldo hakuwa katika kiwango bora huku Benzema na Bale wakionyesha kiwango kizuri.

Katika hatua hii ya Robo fainali Ronaldo amekuwa mchezaji muhimu kwa los blancos baada ya kuiwezesha klabu hiyo kufuzu katika nusu fainali.

Magoli 5 katika mechi 2 dhidi ya Bayern Munich ni ishara inayoonyesha uhitaji wa staa huyo katika mechi kubwa.

3.wahispania wanawatesa sana Wajerumani.
Bayern Munich wamepoteza au kuondolewa katika hatua ya mtoano na Vilabu vya Spain katika misimu 4 mfululizo.Wameondolewa na Barcelona Mara 1,Real madrid 2 na Atletico Madrid Mara 1.

Hii inadhihirisha ubora wa vilabu vya Hispania katika michuano ya ulaya.

4.Marcelo katika kiwango bora.
Hakuna ubishi katika mabeki bora wa pembeni wenye uwezo wa kulinda na Kushambulia Marcelo amekuwa katika kiwango bora kwa miaka kadhaaa.

Aliweza kuokoa mpira uliokuwa unatinga wavuni,Kumdhibiti Robben na kutengeneza goli akipasau safu ya ulinzi ya Bayern Munich.

5.Isco ana vitu adimu miguuni mwake.
Isco ni mzuri katika kuanzisha mashambulizi na kuchezesha timu akitokea nyuma .Kuanze kwake kulikuwa na Advantage kwa Real madrid aliwapa wanachohitaji.

6.Kadi Nyekundu ya vidal haikuwa sahihi

Ahsanteni

LIGI DHAIFU NI IPI??

Na Timotheo john

Kuna tofauti kubwa kati ya kuwa ligi bora na kuwa na timu bora.Binafsi ninaamini kuwa timu bora ni ile iliyobalansi na yenye wachezaji wa ushindani.

Kuwa na mashabiki wengi hakufanyi kitu kuwa bora walau Ubora wa timu sio ligi kuwa na mashabiki wengi walau nilitamani kuzungumza hilo lakini acha niende huku je ni kweli la liga ni ligi dhaifu?

Udhaifu wa ligi upo wapi?? Uwezo wa Barcelona na Real Madrid kutwaa ubingwa Mara nyingi zaidi katika kipindi cha miaka 15.Vipi kuhusu Bundesliga,ligi ya uholanzi au hata Italy ambako Juventus wametwaa Mara 4 mfululizo?

Kutwaa ubingwa Mara nyingi katika ligi flank kunaashiria udhaifu wa ligi?? Kwa mfano hapa Tanzania kuanzia mwaka 2012 wametwaa Mara 3 je ni ligi dhaifu au wapinzani dhaifu??

Kwa muda sasa kumekuwa na maneno kuwa umwamba wa Real Madrid na Barcelona kunafanya ligi hiyo kuonekana dhaifu.Hoja inakuja kwa hiyo tunajaji ubora wa Messi na Ronaldo katika ligi dhaifu???

Ubora wao ninautazama katika michuano ya ulaya katika miaka 5 wanetwaa kombe hilo Mara tatu na wamekuwa wakifanya vyema katika michuano hiyo na Ueropa league.Je michuano hiyo kuna timu dhaifu pia?

Siamini ninaamini kwa kipindi cha Nyuma walau vilabu  toka vilikuwa na Wachezaji wa kiushindani na daraja la dunia.

Sunday, April 16, 2017

UCHAMBUZI:MAN UTD V CHELSEA

Na Timotheo john

MAMBO NILIYOYAONA MANCHESTER UNITED V CHELSEA

1.Safu Mbovu ya ushambuliaji ya Chelsea.
Chelsea walikuwa na safu mbovu ya ushambuliaji iliyofeli katika kila kitu kujaribu kufunga.kwa kipindi cha kwanza Chelsea walipiga shuti moja golini mwa Manchester united.Idara ya ulinzi ya Manchester united haikuwaruhusu Chelsea kulenga lango lao

Kuna muda Costa alitaka kuwatoa mchezoni Rojo na Bailly lakini walimshitukia.

Chelsea hawakutwngeneza nafasi za kufunga tofauti na Manchester united ambao walionekana kuwa na uwezo huo.

2.Fellain alikuwa mtu sahihi Katika idara ya kiungo.
Mara chache wanadamu husema ukweli kama kuna mtu aliyekuwa katika kiwango bora basi ni Fellain aliwapa Manchester united kila kitu wanachohitaji alikaba aliweza kusambaza mipira.

Nafikiri plan ya Jose ilikuwa ni kumkaba mipira ya juu na Fellain alifanikiwa.Ndiye aliyewapa Manchester united nishati ya kujilinda na kushambulia.

3.Jose alifaulu plan zake.
Alimumpanga Herrera kwa ajili ya kumkaba Hazard na Herrera alifanikiwa katika hilo (alimkaba Hazard katika eneo lolote ambap yupo.

Plan ya pili ilikuwa ni Kutowaruhusu Chelsea kumiliki mpira maana wangeleta madhara kwa Manchester united .Wangeutumia jinsi wanavyotaka wao.

4.Rashford katika kiwango bora.
Mapema kabla ya kufunga goli alipata nafasi lakini alipiga mpira nje.Baadaye akafunga goli ambalo lilimpa ujasiri.

Mbali na kufunga Aliweza kutengeneza nafasi kadhaaa za kufunga ambazo hazikutumiwa ipasavyo.Alitengeneza presha kwa walinzi wa Chelsea kila alipokuwa na mpira.

KIPI KINATUFELISHA UGENINI KIMATAIFA?

Na Msalaba Benard

Nipo naendelea kutafakari ushiriki wa timu zetu kunako michuano mbalimbali.

Nipo najaribu kubainisha ni mambo gani yanatutesa hata hatufiki mbali.

Kuna mengi mengine mtayasema wadau ila kwa upande wangu ningependa kudodosa hili la mechi za ugenini.

Nimebaini mara kadhaa tunafanya vema hapa nyumbani ila tunateseka ugenini.

si tu kwa idadi tu ya goli tunazofungwa bali pia 'Performance' yetu (viwango vya timu zetu vikiwa ugenini)

Mbaya zaidi nimebaini hatutumii vema mechi za nyumbani na wakati mwingine tunapumbazwa na wageni wetu.

Tutawashambulia tunakosa nafasi za wazi, tutapata ushindi mwembamba ama sare kisha tutajifariji kungoja miujiza ugenini.

Ona, Mara chache wageni watafunguka wanapocheza hapa. Watatushambulia mara moja moja hususani wakishafungwa.

Ona, Mara chache wageni watacheza kwa kasi. Muda mwingi watajiangusha na kulalama na mwamuzi. Kumbe wanatuzuga.

Ona, Mara chache watatuonesha uwezo wao ambao sio halisi ila huo mtiti wa mechi za ugenini si wa kawaida.

Ona, Watatukimbiza na kutushambulia, wale wale ila hawatoanguka anguka, muda wote wataonesha kiu ya kutufunga.

Kuna mdau kanambia Yanga hawawezi waarabu labda angekuwa Simba nimemkatalia.

Nimemwambia ni sawa nakubali Simba hujitahidi ila bado anateseka mechi za ugenini, hususani zile zile dhidi ya timu za kaskazini.

Nimemsisitizia Si Simba, si Yanga, si Azam si Taifa Stars mechi za ugenini zinatutesa.

Ona, Ni mechi chache utasifia 'performances' yetu ugenini.

Tizama, Mara nyingi zote zitafungwa na wakisharejea tutasikia wakilia fitina na figisu.

Binafsi, kwa miaka 10 ilopita performance bora zaidi kwa timu zetu Uarabuni ni ile ya Yanga na Al Ahly 2015.

Japo walitolewa lakini walicheza na wadau wao wakaridhika na kusuuzika mioyo Yao.

Kuna mdau kanambia hukuiona Simba ilipomnyoa Es Setif? Nimemkumbusha Simba waliteseka sana siku ile.

Nimekumbusha kilichoisaidia simba iliingia Algeria na faida ya goli 2 kisha wakangoja jaribio la Emmanuel Okwi lililozaa faida ya goli la ugenini dk za majeruhi.

Nimekumbusha pia 2012 Simba alimfunga Al Shendy 3-0 hapa akafa 3-0 tena dk 45 za pili za ugenini kisha akatolewa kwa penati.

Nimekumbusha 2011, Simba alimvua Ubingwa wa Afrika TP Mazembe kwa kanuni akapangwa na Wydad Casablanca akapigwa 3-0. Goli zote zikifungwa dk 5 za mwisho.

Nimekumbusha tena mnamo 2009, Simba alimnyoa Harras El Hadood 2-0 taifa, akaenda akanyongwa 5-1 Ugenini.

Anyway niseme tu si lengo la kijimakala hiki kulinganisha rekodi za Yanga na Simba bali nakusudia tutafakari namna vilabu vyetu vinavyojiandaa na kuzikabili  za ugenini. Hususani zile za kasikazini.

Kwenu benchi la ufundi na viongozi Nanyi mjue ni wakati wa kuwa na mipango thabiti. timu zetu ziandaeni kikamilifu.

Msisite hata kuomba ushauri kwa wale waloshiriki tulipofanya vizuri huko Uarabuni.

Jipangeni amueni tukijizatiti tunaweza. Ni nani hakumbuki Simba ilisimama kidété ikawatoa Zamalek kwao 2003?

Ni nani kasahau Yanga nusura amuumbue Al Ahly msimu Ulopita?

Ni nani hakumbuki Yanga ilivyokaza mpaka kutolewa kwa matuta na Al Ahly 2014?

Ama ni nani hakumbuki Yanga hiyo hiyo ilivyojaribia kuiduwaza Étoile du sahel 2015?

Anyway, tusiishie kuwa watu wa kumbukumbu. Tuamue, tufanye kweli. Naomba kuwasilisha.

UCHAMBUZI JUVENTUS V BARCELONA

JUVENTUS V BARCELONA

MAMBO NILIYOYAONA KATIKA MCHEZO HUU

1.Juventus wana team work nzuri
Achana na kucheza kwa kila mtu kwa uwezo wake (individual work) linapokuja suala la kucheza as team work juventus walicheza vyema kuna Kipindi hata mshambuliaji wao Manduzikc alifanya Defense role instead of attacking the enemy team.

2.Cuadrado,Manduzikc,Dyabala na Higuain waliwatesa Barcelona.

Achana na ubora wa Kipa wala viungo wa juventus kitu kingine kilichowapa shida Barcelona ni jinsi ya kuwakaba hawa watu wanne .Waliweza kupanda kwa pamoja kushambulia hali iliyotengeneza presha kubwa katika safu ya ulinzi ya Barcelona.

Goli la kwanza la Juventus ilikuwa ni 8 barce players against those players mentioned above ,Umakini mkubwa uliwawezesha kupata goli hilo

Pia walitengeneza nafasi kadhaa japo hazikuweza kutumika vyema.

3.Dyabala ana taswira nyingine katika soka la ulaya
Msimu uliopita walikuwa na Paul pogba walicheza vizuri.Msimu huu kazidi kutuonyesha taswira tofauti.Alikuwa makini kila anapokuwa na mpira alipiga mashuti 3 huku akifunga magoli 2.

Kuelekea mchezo wa pili atatazamwa sanw pale Nou camp.

4.Ukabaji wa Juventus uliwatesa Barcelona.

Juventus waliwakaba Barcelona kuanzia juu kitu kilichowafanya Barcelona kushindwa kucheza kwa kujiachia na Barcelona kushambulia kuanzia nyuma.

5.Bosquets ni mchezaji muhimu Barcelona.
Kumkosa Bosquets ilikuwa tatizo kwa Barcelona kukiwafanya kuwa dhaifu sana.Kumbuka Barcelona walikuwa wanacheza na moja kati ya timu iliyokamilika barani ulaya.

6.Uzoefu wa Juventus utawapa shida Barcelona Nou camp.
Katika mechi 4 Barcelona hawajashida Turin (sare  2 na kupoteza 2) .Pia Juventus wanauzoefu na michuano hii uongozi wa 3- 0 ni faida kwao.

Ahsanteni

UCHAMBUZI BAYERN MUNICH V REAL MADRID

NIMEYAONA HAYA BAYERN MUNICH V REAL MADRID

1.Real Madrid ndiyo timu inayowapa shida Bayern Munich Allianz alena.
Mara ya Mwisho Bayern kupoteza katika uwanja wa nyumbani ilikuwa mwaka 2014 walifungwa 4-0 na Real Madrid.

Timu yoyote ilikuwa ikifika hapo inafungwa tumeshuhudia Arsenal,Barcelona,Benfica na timu nyinginezo zikifungwa lakini Real Madrid wanafanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-1 ni timu iliyoipa shida Bayern Munich wakiwa nyumbani allianz arena.

2.Santiago Bernabeu kunaweza kusiwe pahala sahihi machoni Mwa Bayern Munich.
Msimu huu kuna timu mbili ambazo hazijapoteza mchezo wowote ule katika michuano ya ulaya ni Real maadrid na Juventus.

Ugumu wa kutopoteza mechi yeyote kutawapa shida Bayern Munich ukiongeza na uongozi wa 2-1 wa Real Madrid.

3.Pengo la Lewandowiski lilionekana
Lewandowiski msimu huu kafunga magoli 48 katika mechi 49 kwa klabu na timu ya taifa.Amekuwa muhimili muhiku katika safu ya ushambuliaji ya Bayern Munich katika michuano yote.

Kwa Jana nafasi yake alicheza Muller ambaye hakuwa katika kiwango bora pengo la Robert Lewandowski lilionekana.

4.Real Madrid Wanahitaji ubora wa BBC
Washambuliaji watatu wa Real Madrid Benzema,Bale na Ronaldo hawajawa katika kiwango bora msimu huu ukifananisha na cha msimu wa 2014/2015.

Gareth bale ameandamwa sana na Majeraha,Ronaldo umri unamtupa mkono.

Kwa kioindi cha pili Real Madrid Cr7 alirudi kwa kufunga magoli mawili kwa Real Madrid.Real madrid kufanya cyema katika michuano hii ni lazima safi yao ya ushambuliaji irejeshe makali yao.

5.Safu ya Ulinzi ya Bayern Munich soft.
Bayern Munich wanakuwa soft sana wanapokuyana na timu inayocheza soka la kushambulia.Shukrani Zimwendee Manuer Neur kwa jinsi alivyoweza kuokoa michomo ya hatari.

Ahsanteni

Friday, December 30, 2016

NINACHOKIAMINI TIMOTH..SCHNEIDERLIN ANGUKO LINGINE MANCHESTER UNITED

NINACHOKIAMINI TIMOTH

SCHNEIDERLIN ANGUKO LINGINE MANCHESTER UNITED

Na Timotheo John

Manchester united kwa sasa wameishataja wachezaji ambao watauzwa kwa mwezi ujao katika dirisha dogo jina mojawapo ni la kiungo Morgan schneiderlin aliyesajiliwa na Louis van Gaal msimu uliopita.

Morgan anatajwa kuwa kama ni moja ya Viungo waliokamilika hasa katika idara ya kiungo akiwa kama kiungo Mkabaji (Mkata umeme).

Morgan katika michezo 32 aliyoichezea Manchester united amefanikiwa kufunga goli 1 alifunga dhidi ya Everton.Kiungo huyo hakupewa nafasi lakini alikuwa anaifanya kazi kubwa katikati ya Dimba.

Wakati msimu uliopita Manchester united walipoteza michezo 4 mfululizo katika kipindi cha miaka 50 iliyopita walifanya hivyo.

Usajili wa kiungo Paul pogba kutokea juventus umekuwa na tija huku Kwa sasa katika eneo la kiungo wakipagwa Herrera.Carrick na Pogba .Jukumu kubwa la Pogba ni kuchezesha timu.

Kwanini Pogba anashine ?? Ni kutokana na sasa jukumu lake kubwa ni kuchezesha timu (japo anaweza kuwa kama kiungo mshambuliaji).Kazi kubwa ya Manchester united ipo miguuni mwa Carrick.

Kabla ya ujio huo wa pogba Manchester united walikuwa na Carrick pamoja na Morgan katika eneo la kiungo hasa ukabaji.Ujio wa pogba umeongeza idadi ya viungo wakabaji.

Umri wa Carrick miaka 35 amekuwa tegemeo Manchester united kwa muda mrefu sio mda atatundika daruga.Je Manchester united wanamhitaji Morgan katika hili??

Ndiyo.Manchester united wanamhitaji Morgan katika kipindi hiki ambapo Carrick kageuka kuwa Msingi wa Manchester united Morgan anaweza kuwa mbadala wa Carrick kwa 80% endapo carrick litampta lolote.

Kiungo ya Manchester united inaweza kuundwa na Morgan Schneiderlin akiwa kama mkabaji Ander Herrera na Paul pogba bado wakafanya vyema.Au kama Jose atakuwa anataka kujilinda anaweza kuwatumia pogbs na Morgan kama wakabaji.

Binafsi naamini kumuachia Schneiderlin aondoke january litakuwa anguko kwa manchester united kuanzia Umri wake hadi Jukumu lake uwanjani.Na viungo wa stahili hii wamepotea duniani.

Unaikumbuka southampton ya mkabaji Morgan na Victor wanyama?? Ilikuwaje??

Wednesday, December 28, 2016

TATIZO JAMIE VARDY HAMJUI NTUYABALINE

Na Green osward

Msimu uliopita mwezi kama huu, kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.. Haikukuhitaji uvae miwani ya macho ili uitazame Leicester city ipo nafasi ya ngapi.. Walikuwa juu ya msimamo wakisheherekea sikuu ya Christmas uku wakiwa na point zilizowahakikikishia kuwepo kwenye top four..

Ndoto zakushuka daraja ndani ya vichwa vyao.. Zilikuwa zimeyeyuka ghafla mithili ya siagi iliyowekwa kwenye sufuria lililotengwa kwenye jiko la gesi... Walikuwa kwenye dunia nyingine kifikra,.. Dunia liyowapa usingizi wa kuota kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England...

Ilikuwa ni ndoto ambayo ilibidi umuwekee mtutu wa bunduki ubongoni shabiki wa Arsenal, Manchester United, Liverpool na Chelsea.. Ili aisadiki ndoto ya Leicester city kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England kuwa inaweza kuwa kweli ifikapo mwezi may...

Msimu uliopita mwezi kama huu Jamie Vardy alikuwa ana goal 14.. Akiwa ameweka record yakuwa mchezaji wa kwanza kufunga goal 11 mfululizo kwenye ligi kuu ya England.. Ligi kuu ya England aliigeuza mateka wake, akawa anaisurubu anavyotaka... Miguu ya Vardy ilikuwa kwenye shabaha ya kutisha.. Miguu yake haikuwa na huruma kila alipotaka kuzizuru timu pinzani..

Old Trafford, Emirates, Anfield, Stamford bridge, na viwanja vingine vikubwa.. Ni sehemu ambazo nyavu zake zilipata kushuhudia ukatili unaoutenda Jamie Vardy kwa kutumia miguu yake..
Kila week end miguu ya Vardy ilikuwa inaingia uwanjani uku ikiwa ndani ya viatu vya Lionel Messi na Christian Ronaldo..

Dunia iliyonajisiwa na dhambi haijawahi kumtengenezea furaha ya kudumu mwanadamu yoyote ndani ya moyo wake..Msimu huu nyakati tamu zimevunja urafiki na miguu ya Jamie Vardy..Misuli ya mapaja yake imehasi kutoa ushirikiano namagoti... Na Tabasamu limekuwa adimu kwenye uso wake zaidi ya pembe za faru John...

Ktk orodha ya wafungaji 15 bora ktk ligi kuu ya England.. Jina la Vardy huwezi kuliona hata kama utatumia darubini waliyokuwa wanatumia makomandoo wa Marekani kwenye operations ya kumsaka Osama bin Laden...Idadi ya Goal alizofunga mpaka sasa, ..Inazidiwa hata na idadi ya vidole vya mkono wa mtoto mchanga aliyetoka Leba... Magoal yamemkimbia zaidi ya kibaka aliyeichoropoa shingo yake kwenye tairi la moto...

Leo Leicester ipo mahututi kwenye msimamo wa ligi.. Inaupigania uhai wakubaki ligi kuu ikiwa hospital ya king power chini ya Doctor Vardy... Doctor ambaye naye miguu yake imepata upofu.. Na hawezi kuziona vema tena nyavu za timu pinzani.. Hizi ni nyakati zinazozalisha mamillion ya Majuto kwenye moyo wavardy.. Akijuta kwanini aliikataa ofa ya kujiunga ARSENAL. . Sema hawezi kukiri kuieleza dunia. Maana itakuwa sawa nakujivua nguo sokoni..

January 11 Vardy ataitimiza miaka 30.. Umri ambao mashabiki wa soka huwa wanaizika adabu nakuanza kumtambua mchezaji kama mtu mzee..Na hakuna timu yoyote kubwa inayoweza kuweka chambo kisha kutupa ndoano kwenye mdomo wa Jamie Vardy.. Kutakiwa na Arsenal.. Nafasi kama ile huwa inatokea mara moja tu kwenye maisha ya mwanadamu..

Nafasi kama ile aliipata dada yangu JAQLEEN NTUYABALIWE.. Alipobaki yeye na Mzee Mengi akamfunga mzee goal la ndoa.. Vardy ATAJUTA kuikataa nafasi ya kuichezea Arsenal mpaka siku atayolala ndani ya shimo liitwalo KABURI. ''

0715 035 836

Tuesday, December 20, 2016

WACHINA TWENDENI TUSIRUDI NYUMA

Na Timotheo s john

Kuna mwanadamu mmoja alishawahi kusema kinachomfanya mtu kufanikiwa ni kwanza kujielewa,Kujituma,Kuwa mbunifu na kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa.Huenda mwanadamu huyo alikuwa sahihi lakini kuna kitu kimoja alisahau kukitaja kuwa ni kutokata tamaa pale unapohitaji kufanikiwa huku malengo ukiwa umejiwekea na Mambo yake manne umetimiza.

Miaka 200-350 (karne mbili hadi nne zilizopita ) Uingereza ndiyo ilikuwa Dora tajiri zaidi duniani kutokana na shughuli mbalimbali kama vile Biashara hasa ya viwanda.Kwa kipindi hiki sio Marekani wala China alifikia nusu ya mafanikio hayo.Miaka ikasonga Majirani (Ufaransa,Italy na Ujerumani Wakarudi nyuma wakaiba teknolojia ya mwingereza na wakaiboresha zaidi ).Unajua kipi kilitokea???

Uingereza alizidi kudidimia baadaye yaani kufikia mwaka 1776 mmarekani alipata Uhuru kutika kwa Mwingereza .Waingereza hapa wananifurahisha kwa mambo kadhaa mojawapo walikuwa na viwanda Vingi nchini Marekani baada ya Marekani kupata Uhuru Uingereza ilupoteza viwanda vile hivi walijua nchi ya kwao ile??? Kwa sasa wamebakiza historian tu kuwa wamewahi kuwa wazalishaji na taifa tajiri zaidi duniani.

Mmarekani kwa sasa kiuchumi yupo katika climax (hauwezi kuongezeka bali unaweza kupungua) kwa sasa wao hawajali hiyo wanafikiria kuhama dunia hii tulitopo kwa sababu sio pahala salama mi nasubiri tu unajua kwa mini?? Muda ndio utaamu kama karne kadhaa zilizopita.

Kuna nyakati mwanadamu anaishi anavyotaka yeye.Kuna kipindi Monaco walinyanyasa sana sio kimpira Bali kutumia pesa ..Kuna Nyakati hakuna timu ambayo ilipenda kushindana na real Madrid katika usajili pia kuna nyakati Bayern Munich anharibu radha ya bundesliga kutokana na Pesa zake.

Kuna nyakati mwanadamu analipwa zaidi ya 1.5 billions za kitanzania katika soka hakuna anayehoji zaidi wale wakubwa kuulizana inakuwaje hapa?? Jamaa wamekuja tena kwa kasi sina si wengine wamefanya mengi katika teknolojia..uchumi na sasa Wamegundua huu ni wakati WA kuingia katika soka.Wanalila vizuri wanajua kujitangaza maisha yanasonga.

Unamkumbuka Carlos tevez yule jamaa WA west ham...Manchester city...Manchester united na juventus juzi akiwa kwa watoto WA Ghetto alikuwa akiwaaga rasmi anaenda china  kunusa pesa.Ndiyo ni Suala la Muda tu .

Tevez atakuwa akilipwa £615,000 pauni kwa wiki ambazo ni sawa na 1.84 5billions za kitanzania nani anajali pia atakuwa akiingiza £31. 98millions per year zaidi ya Messi na Ronaldo

Kama oscar emoeba dos santos akijunga huyu atakuwa akilipwa £400000 kwa wiki sawa na 1.2 billions za kitanzania maisha yanataka nini zaidi ??? kuna hawa jamaa wanaitwa Hebei wao wanamtaka sanchez watakuwa wakimlila pauni 500000.

Wakati fujo China zinaendelea  katika  soka Hebei wanekuja tens wanamtaka Messi unaujua mshahara wake?? Wamemwambia watampatia £100 millions per year hii ni Mara  3ya zile ambazo Tevez atakuwa akilipwa pale Shaghai Shenua Sipg maisha yanataka nini zaidi???

Kwa bahati nzuri rais wao Xi jinoing ni mpenda mchezo wa fooball.Wachina wanekuja nyakati hizi wanalipa vizuri kuna kitu wanakitaka karika dunia yenye ubabe wa kila aina.Kwa sasa Macho yangu yapo ulaya lakini akiki na masikio IPO china

Kwa bahati nzuri kwa sasa China ndiye mzalishaji mkuu WA bidhaa nyingi hapa duniani amechoka huko alipo anataka kuja huku acha tusubiri safari hii ya Wetlands .Mpaka sasa wanasifa moja ya kujituma kuelekea mafanikio acha tusubiri Mudaa utawahukumu.

Tuesday, December 13, 2016

HERRERA UMEMUONA CARRICK?


HERRERA UMEMUONA CARRICK?





Manchester united Leo wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 1-0 dhidi ya Tottenham hotspurs wakiwa nyumbani Old Trafford ,Mikhitaryan akiwa ndiye mfungaji wa goli hilo pekee.

Huu ni ushindi wa kwanza wa Manchester united katika ligi tangu September 24 kumbuka kabla ya Leo Manchester walikuwa hawajashinda hata mchezo mmoja.

Kuna kitu kimoja nataka nikukumbushe Michael carrick alihama Tottenham na kutua Manchester united mwaka 2007 na kuja kuwa muhimili mkubwa hasa katika eneo la Kiungo.

Baada ya kuondoka Paul scholes Manchester united hawakuweza kupata aina ya kiungo wake lakini bado carrick alionekana walau anaweza jukumu lile (Hakuwa na uwezo wa Paul)

Carrick ni moja kati ya viungo wakongwe wenye uwezo wa kupiga pasi ndefu na fupi,kukaba ,Kushambulia pia ni kiongozi mzuri awapo uwanjani (mbali na nahodha pia huwa kama Mwalimu)

Viungo wengi wamepita pale Manchester united kama cleverly ,Anderson,Kagawa na wengineo ambao walionekana kufeli lakini kuna mtu anaitwa Ander Herrera ( kiungo muongo)

Achana na Schweinsteiger ,Schneiderlin au Fellain kuna huyu Herrera.Jamaa ni moja kati ya viungo wachache wenye uwezo wa kusakata kabumbu.

Wakati Manchester united wakiwa hawajapoteza mechi 11 (kushinda 9 na sare 2) kila Carrick anapoanza katika kikosi cha timu hiyo.Kwa sasa Jose Anamtumia Herrera na Carrick katika kiungo ya chini ni kama kashinda unajua kwanini????

Kiungo Carrick akiwa mkabaji wakishirikiana vyema na Herrera huku pogba akishambulia Manchester united wanakuwa na uwiano mzuri hasa  ukiwatazama wau hao wanatabia zinazofanana.Idara ya kiungo ya Manchester united inaonekana kubadilika kwa sasa tofauti na mwanzo.

Mwalimu anaweza kumuanzisha Morgan  na Herrera au Carrick na Morgan au Bastian na carrick (hapa umri huwa kikwazo ) au Fellain na Herrera .lakini unajua kwanini Jose kamuamini Herrera??

Herrera kabadilika sana nidhamu ..uwezo na kujituma kwake kumempa namba herrera.Huu ni wakati wake was kutawala eneo la kiungo la timu hiyo.

Sina shaka kuhusu uwezo wake lakini je huyu ndiye mrithi  wa carrick? Kwa sasa kaaminiwa anahitaji kuaminika

TIMOTHEO S JOHN
SIMU 0712563344

UTAWALA WA KIHASPANIOLA KATIKA SOKA LA ULAYA

WAHISPANIA WAMETAWALA SOKA LA ULAYA.WAKATI WA KUJIULIZA Msimu uliopita Seville walitwaa ubingwa wa Ueropa league kwa kuifinga Liverpool 3-1...