Friday, December 30, 2016

NINACHOKIAMINI TIMOTH..SCHNEIDERLIN ANGUKO LINGINE MANCHESTER UNITED

NINACHOKIAMINI TIMOTH

SCHNEIDERLIN ANGUKO LINGINE MANCHESTER UNITED

Na Timotheo John

Manchester united kwa sasa wameishataja wachezaji ambao watauzwa kwa mwezi ujao katika dirisha dogo jina mojawapo ni la kiungo Morgan schneiderlin aliyesajiliwa na Louis van Gaal msimu uliopita.

Morgan anatajwa kuwa kama ni moja ya Viungo waliokamilika hasa katika idara ya kiungo akiwa kama kiungo Mkabaji (Mkata umeme).

Morgan katika michezo 32 aliyoichezea Manchester united amefanikiwa kufunga goli 1 alifunga dhidi ya Everton.Kiungo huyo hakupewa nafasi lakini alikuwa anaifanya kazi kubwa katikati ya Dimba.

Wakati msimu uliopita Manchester united walipoteza michezo 4 mfululizo katika kipindi cha miaka 50 iliyopita walifanya hivyo.

Usajili wa kiungo Paul pogba kutokea juventus umekuwa na tija huku Kwa sasa katika eneo la kiungo wakipagwa Herrera.Carrick na Pogba .Jukumu kubwa la Pogba ni kuchezesha timu.

Kwanini Pogba anashine ?? Ni kutokana na sasa jukumu lake kubwa ni kuchezesha timu (japo anaweza kuwa kama kiungo mshambuliaji).Kazi kubwa ya Manchester united ipo miguuni mwa Carrick.

Kabla ya ujio huo wa pogba Manchester united walikuwa na Carrick pamoja na Morgan katika eneo la kiungo hasa ukabaji.Ujio wa pogba umeongeza idadi ya viungo wakabaji.

Umri wa Carrick miaka 35 amekuwa tegemeo Manchester united kwa muda mrefu sio mda atatundika daruga.Je Manchester united wanamhitaji Morgan katika hili??

Ndiyo.Manchester united wanamhitaji Morgan katika kipindi hiki ambapo Carrick kageuka kuwa Msingi wa Manchester united Morgan anaweza kuwa mbadala wa Carrick kwa 80% endapo carrick litampta lolote.

Kiungo ya Manchester united inaweza kuundwa na Morgan Schneiderlin akiwa kama mkabaji Ander Herrera na Paul pogba bado wakafanya vyema.Au kama Jose atakuwa anataka kujilinda anaweza kuwatumia pogbs na Morgan kama wakabaji.

Binafsi naamini kumuachia Schneiderlin aondoke january litakuwa anguko kwa manchester united kuanzia Umri wake hadi Jukumu lake uwanjani.Na viungo wa stahili hii wamepotea duniani.

Unaikumbuka southampton ya mkabaji Morgan na Victor wanyama?? Ilikuwaje??

Wednesday, December 28, 2016

TATIZO JAMIE VARDY HAMJUI NTUYABALINE

Na Green osward

Msimu uliopita mwezi kama huu, kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.. Haikukuhitaji uvae miwani ya macho ili uitazame Leicester city ipo nafasi ya ngapi.. Walikuwa juu ya msimamo wakisheherekea sikuu ya Christmas uku wakiwa na point zilizowahakikikishia kuwepo kwenye top four..

Ndoto zakushuka daraja ndani ya vichwa vyao.. Zilikuwa zimeyeyuka ghafla mithili ya siagi iliyowekwa kwenye sufuria lililotengwa kwenye jiko la gesi... Walikuwa kwenye dunia nyingine kifikra,.. Dunia liyowapa usingizi wa kuota kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England...

Ilikuwa ni ndoto ambayo ilibidi umuwekee mtutu wa bunduki ubongoni shabiki wa Arsenal, Manchester United, Liverpool na Chelsea.. Ili aisadiki ndoto ya Leicester city kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England kuwa inaweza kuwa kweli ifikapo mwezi may...

Msimu uliopita mwezi kama huu Jamie Vardy alikuwa ana goal 14.. Akiwa ameweka record yakuwa mchezaji wa kwanza kufunga goal 11 mfululizo kwenye ligi kuu ya England.. Ligi kuu ya England aliigeuza mateka wake, akawa anaisurubu anavyotaka... Miguu ya Vardy ilikuwa kwenye shabaha ya kutisha.. Miguu yake haikuwa na huruma kila alipotaka kuzizuru timu pinzani..

Old Trafford, Emirates, Anfield, Stamford bridge, na viwanja vingine vikubwa.. Ni sehemu ambazo nyavu zake zilipata kushuhudia ukatili unaoutenda Jamie Vardy kwa kutumia miguu yake..
Kila week end miguu ya Vardy ilikuwa inaingia uwanjani uku ikiwa ndani ya viatu vya Lionel Messi na Christian Ronaldo..

Dunia iliyonajisiwa na dhambi haijawahi kumtengenezea furaha ya kudumu mwanadamu yoyote ndani ya moyo wake..Msimu huu nyakati tamu zimevunja urafiki na miguu ya Jamie Vardy..Misuli ya mapaja yake imehasi kutoa ushirikiano namagoti... Na Tabasamu limekuwa adimu kwenye uso wake zaidi ya pembe za faru John...

Ktk orodha ya wafungaji 15 bora ktk ligi kuu ya England.. Jina la Vardy huwezi kuliona hata kama utatumia darubini waliyokuwa wanatumia makomandoo wa Marekani kwenye operations ya kumsaka Osama bin Laden...Idadi ya Goal alizofunga mpaka sasa, ..Inazidiwa hata na idadi ya vidole vya mkono wa mtoto mchanga aliyetoka Leba... Magoal yamemkimbia zaidi ya kibaka aliyeichoropoa shingo yake kwenye tairi la moto...

Leo Leicester ipo mahututi kwenye msimamo wa ligi.. Inaupigania uhai wakubaki ligi kuu ikiwa hospital ya king power chini ya Doctor Vardy... Doctor ambaye naye miguu yake imepata upofu.. Na hawezi kuziona vema tena nyavu za timu pinzani.. Hizi ni nyakati zinazozalisha mamillion ya Majuto kwenye moyo wavardy.. Akijuta kwanini aliikataa ofa ya kujiunga ARSENAL. . Sema hawezi kukiri kuieleza dunia. Maana itakuwa sawa nakujivua nguo sokoni..

January 11 Vardy ataitimiza miaka 30.. Umri ambao mashabiki wa soka huwa wanaizika adabu nakuanza kumtambua mchezaji kama mtu mzee..Na hakuna timu yoyote kubwa inayoweza kuweka chambo kisha kutupa ndoano kwenye mdomo wa Jamie Vardy.. Kutakiwa na Arsenal.. Nafasi kama ile huwa inatokea mara moja tu kwenye maisha ya mwanadamu..

Nafasi kama ile aliipata dada yangu JAQLEEN NTUYABALIWE.. Alipobaki yeye na Mzee Mengi akamfunga mzee goal la ndoa.. Vardy ATAJUTA kuikataa nafasi ya kuichezea Arsenal mpaka siku atayolala ndani ya shimo liitwalo KABURI. ''

0715 035 836

Tuesday, December 20, 2016

WACHINA TWENDENI TUSIRUDI NYUMA

Na Timotheo s john

Kuna mwanadamu mmoja alishawahi kusema kinachomfanya mtu kufanikiwa ni kwanza kujielewa,Kujituma,Kuwa mbunifu na kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa.Huenda mwanadamu huyo alikuwa sahihi lakini kuna kitu kimoja alisahau kukitaja kuwa ni kutokata tamaa pale unapohitaji kufanikiwa huku malengo ukiwa umejiwekea na Mambo yake manne umetimiza.

Miaka 200-350 (karne mbili hadi nne zilizopita ) Uingereza ndiyo ilikuwa Dora tajiri zaidi duniani kutokana na shughuli mbalimbali kama vile Biashara hasa ya viwanda.Kwa kipindi hiki sio Marekani wala China alifikia nusu ya mafanikio hayo.Miaka ikasonga Majirani (Ufaransa,Italy na Ujerumani Wakarudi nyuma wakaiba teknolojia ya mwingereza na wakaiboresha zaidi ).Unajua kipi kilitokea???

Uingereza alizidi kudidimia baadaye yaani kufikia mwaka 1776 mmarekani alipata Uhuru kutika kwa Mwingereza .Waingereza hapa wananifurahisha kwa mambo kadhaa mojawapo walikuwa na viwanda Vingi nchini Marekani baada ya Marekani kupata Uhuru Uingereza ilupoteza viwanda vile hivi walijua nchi ya kwao ile??? Kwa sasa wamebakiza historian tu kuwa wamewahi kuwa wazalishaji na taifa tajiri zaidi duniani.

Mmarekani kwa sasa kiuchumi yupo katika climax (hauwezi kuongezeka bali unaweza kupungua) kwa sasa wao hawajali hiyo wanafikiria kuhama dunia hii tulitopo kwa sababu sio pahala salama mi nasubiri tu unajua kwa mini?? Muda ndio utaamu kama karne kadhaa zilizopita.

Kuna nyakati mwanadamu anaishi anavyotaka yeye.Kuna kipindi Monaco walinyanyasa sana sio kimpira Bali kutumia pesa ..Kuna Nyakati hakuna timu ambayo ilipenda kushindana na real Madrid katika usajili pia kuna nyakati Bayern Munich anharibu radha ya bundesliga kutokana na Pesa zake.

Kuna nyakati mwanadamu analipwa zaidi ya 1.5 billions za kitanzania katika soka hakuna anayehoji zaidi wale wakubwa kuulizana inakuwaje hapa?? Jamaa wamekuja tena kwa kasi sina si wengine wamefanya mengi katika teknolojia..uchumi na sasa Wamegundua huu ni wakati WA kuingia katika soka.Wanalila vizuri wanajua kujitangaza maisha yanasonga.

Unamkumbuka Carlos tevez yule jamaa WA west ham...Manchester city...Manchester united na juventus juzi akiwa kwa watoto WA Ghetto alikuwa akiwaaga rasmi anaenda china  kunusa pesa.Ndiyo ni Suala la Muda tu .

Tevez atakuwa akilipwa £615,000 pauni kwa wiki ambazo ni sawa na 1.84 5billions za kitanzania nani anajali pia atakuwa akiingiza £31. 98millions per year zaidi ya Messi na Ronaldo

Kama oscar emoeba dos santos akijunga huyu atakuwa akilipwa £400000 kwa wiki sawa na 1.2 billions za kitanzania maisha yanataka nini zaidi ??? kuna hawa jamaa wanaitwa Hebei wao wanamtaka sanchez watakuwa wakimlila pauni 500000.

Wakati fujo China zinaendelea  katika  soka Hebei wanekuja tens wanamtaka Messi unaujua mshahara wake?? Wamemwambia watampatia £100 millions per year hii ni Mara  3ya zile ambazo Tevez atakuwa akilipwa pale Shaghai Shenua Sipg maisha yanataka nini zaidi???

Kwa bahati nzuri rais wao Xi jinoing ni mpenda mchezo wa fooball.Wachina wanekuja nyakati hizi wanalipa vizuri kuna kitu wanakitaka karika dunia yenye ubabe wa kila aina.Kwa sasa Macho yangu yapo ulaya lakini akiki na masikio IPO china

Kwa bahati nzuri kwa sasa China ndiye mzalishaji mkuu WA bidhaa nyingi hapa duniani amechoka huko alipo anataka kuja huku acha tusubiri safari hii ya Wetlands .Mpaka sasa wanasifa moja ya kujituma kuelekea mafanikio acha tusubiri Mudaa utawahukumu.

Tuesday, December 13, 2016

HERRERA UMEMUONA CARRICK?


HERRERA UMEMUONA CARRICK?





Manchester united Leo wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 1-0 dhidi ya Tottenham hotspurs wakiwa nyumbani Old Trafford ,Mikhitaryan akiwa ndiye mfungaji wa goli hilo pekee.

Huu ni ushindi wa kwanza wa Manchester united katika ligi tangu September 24 kumbuka kabla ya Leo Manchester walikuwa hawajashinda hata mchezo mmoja.

Kuna kitu kimoja nataka nikukumbushe Michael carrick alihama Tottenham na kutua Manchester united mwaka 2007 na kuja kuwa muhimili mkubwa hasa katika eneo la Kiungo.

Baada ya kuondoka Paul scholes Manchester united hawakuweza kupata aina ya kiungo wake lakini bado carrick alionekana walau anaweza jukumu lile (Hakuwa na uwezo wa Paul)

Carrick ni moja kati ya viungo wakongwe wenye uwezo wa kupiga pasi ndefu na fupi,kukaba ,Kushambulia pia ni kiongozi mzuri awapo uwanjani (mbali na nahodha pia huwa kama Mwalimu)

Viungo wengi wamepita pale Manchester united kama cleverly ,Anderson,Kagawa na wengineo ambao walionekana kufeli lakini kuna mtu anaitwa Ander Herrera ( kiungo muongo)

Achana na Schweinsteiger ,Schneiderlin au Fellain kuna huyu Herrera.Jamaa ni moja kati ya viungo wachache wenye uwezo wa kusakata kabumbu.

Wakati Manchester united wakiwa hawajapoteza mechi 11 (kushinda 9 na sare 2) kila Carrick anapoanza katika kikosi cha timu hiyo.Kwa sasa Jose Anamtumia Herrera na Carrick katika kiungo ya chini ni kama kashinda unajua kwanini????

Kiungo Carrick akiwa mkabaji wakishirikiana vyema na Herrera huku pogba akishambulia Manchester united wanakuwa na uwiano mzuri hasa  ukiwatazama wau hao wanatabia zinazofanana.Idara ya kiungo ya Manchester united inaonekana kubadilika kwa sasa tofauti na mwanzo.

Mwalimu anaweza kumuanzisha Morgan  na Herrera au Carrick na Morgan au Bastian na carrick (hapa umri huwa kikwazo ) au Fellain na Herrera .lakini unajua kwanini Jose kamuamini Herrera??

Herrera kabadilika sana nidhamu ..uwezo na kujituma kwake kumempa namba herrera.Huu ni wakati wake was kutawala eneo la kiungo la timu hiyo.

Sina shaka kuhusu uwezo wake lakini je huyu ndiye mrithi  wa carrick? Kwa sasa kaaminiwa anahitaji kuaminika

TIMOTHEO S JOHN
SIMU 0712563344

Sunday, July 10, 2016

MAMBO UNAYOTAKIWA KUJUA KUELEKEA FAINALI YA UERO

Na Timotheo S John

-Hii ni Mara ya 4 kwa timu hizi kukutana katika mashindano makubwa huku Ufaransa wakiwa wameshinda mechi 3 zote ni katika
nusu fainali ya Uero 1994,Uero 2000 na kombe la dunia 2006

-Ureno wamecheza mechi nyingi za michuano ya ulaya bila kushinda (34) huku Cristiano Ronaldo aliyesawa magoli kwa ufungaji na
platin ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi (20)

-Ureno hawajafungwa katika mechi 13 chini ya Fernando Santos (kushinda 9 na sare 4) huku ushindi dhidi ya wales ukiwa ni ushindi wao
wa kwanza kushinda zaidi ya goli 1.

-Ureno wamefungwa goli 1 katika hatua ya mtoano kwenye mechi 5 za karibuni.Mwaka huu walifungwa na Poland.

-Ufaransa hawajapoteza katika mechi 18 walizocheza katika ardhi ya nyumbani (kushinda 16 sare 2) Mara ya mwisho kupoteza ilikuwa July mwaka 1960 dhidi ya Czechoslovakia.

-Ufaransa ndio timu pekee iliyotwaa kombe hili Mara 3 sawa na Hispania pia na ujerumani.

-Kama ufaransa watatwaa kombe hili Didier Deschamps atakuwa mtu wa pili kutwaa kombe hili akiwa mchezaji pia kocha wa kwanza kufanya hivyo ni Bergi Vogets kutoka ujerumani

Thursday, May 19, 2016

JICHO LANGU VIWANJANI HISPANIA WATAWALA WAPYA WASOKA BARANI ULAYA

Mawasiliano
Johntimotheo6@gmail.com
Simu:0712563344

Na Timotheo John

Timu ya Seville imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ueropa ligi kwa Mara ya 3 mfululizo baada ya kuifunga Liverpool kwenye mchezo wa fainali 3-1 hapo Jana nchini Uswisi.Hii ni Mara ya 3 kwa timu hiyo kutwaa ubingwamfululizo kwa kuzifunga timu za
Dnipro,Benfica na Liverpool .

Wakati Seville wakifanikiwa kutwaa ubingwa Mei 28 nchini Italia itafanyika fainaliinayowakutanisha vigogo kutoka Hispania (Real Madrid na Atletico Madrid) ambapo Real Madrid wamefuzu kwa kuwatoa Manchester city huku Atletico wakiwatoa Bayern Munich kutoka Ujerumani.

Kwa kutumia viwango ambavyo timu za Hispania zimeonyesha kwenye michuano ya ulaya (uefa na ueropa) ni dhahiri kuwa kwa sasa timu kutoka nchi hiyo zimetawala soka la ulaya katika kipindi cha miaka 5.Usibishe nikuambie. katika miaka 5 timu hizo zimejenga nguzo imara ya utawala wa vilabu barani ulaya.

Katika misimu miwili iliyopita makombe mawili makubwa Uefa na Ueropa zimebeba timu za Hispania.Msimu wa 2013/2014 Real Madrid walitwaa kwa kuifunga Atletico Madrid (kutoka Hispania) huku Seville wakiifunga Benfica na kutwaa Ubingwa wa Ueropa.

Msimu wa 2014/2015 timu ya Barcelona ikifanikiwa kutwaa ubingwa kwa kuifunga Juventus 3-1 pia msimu huo huo Seville walitwaa Ueropa kwa kuifunga timu ya Dnipro.Ina maana katika miaka 2 timu kutoka Hispania zilitwaa kombe la mabingwa ulaya x2 ueropa x2 na super cup x2 (super cup hushirikisha bingwa wa uefa na ueropa).

Na msimu huu tayari Seville wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa ueropa kwa Mara ya 3 mfululizo huku ukiwa ni ubingwa wa 5 kwa ujumla.Ina maana tena msimu huu Makombe 3 yatatua nchini hispania .Mafanikio ya vilabu hivyo vinafanya niamini kuwa timu kutoka hispania ndio watawaka wapya wa soka la ulaya.

Kwa nini timu kama Seville,hufanya vyema katika ueropa na haiwezi kutwaa walau ubingwa wa ligi kuu ya Hispania?? Utagundua kuwa timu hizi zina wachezaji wachache na wenye viwango vya dunia ambao hauwezi kushindanisha na timu zile 3 kubwa (Real Madrid,Barcelona na Atletico Madrid).Kwa mantiki hiyo ni viguku kwa timu hizo kutawala soka la Hispania lakini linapokuja suala la Michuano ya Ueropa ligi huwa wanafanya vyema.

Imani yangu ni kuwa Hispania ndio watawala wa soka la ulaya hii inatokana na mafanikio ya vilabu kutoka nchini humo katika
michuano mikubwa barani ulaya.

Wednesday, May 18, 2016

YANGA YATINGA MAKUNDI LICHA YA KIPIGO CHA 1-0

Klabu ya Yanga imefanikiwa kufuzu kwenye hatua ya makundi ya michuano ya CAF kwa mara ya kwanza tangu walipofanikiwa kufanya hivyo kwa mara ya kwanza na ya mwisho mwaka 1998.

Yanga wamefungwa na Sagrada Esparenca kwa bao 1-0 lakini wamefuzu kwa matokeo ya
jumla (Sagrada Esparenca 1-2 Yanga) hivyo kikosi cha Hans van Pluijm kinasonga mbele
kwenye michuano hiyo ya Afrika.

Mechi ya Yanga dhidi ya Esparanca haikuwa rahisi kama watu wengi walivyotarajia kwasababu hadi kipindi cha kwanza
kinamalizika wachezaji wanne wa Yanga walikuwa tayari wameoneshwa kadi za njano

Haruna Niyonzima, Thabani Kamusoko, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Deogratius Munishi Dida ni baadhi ya wachezaji waliooneshwa kazi za njano kutokana na matukio tofauti ya kinidhamu.

Dida aliibeba Yanga baada ya kudaka
mchomo wa penati zikiwa ni dakika za lala salama na kuendelea kuweka Yanga kwenyenafasi nzuri ya kusonga mbele.

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub Cannavaro alizawadiwa kadi nyekundu dakika za mwisho kabisa za mchezo huo.

ROONEY AWEKA HISTORIA MPYA

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney jana aliweka rekodi nyingine baada kufunga bao lake la 100 katika ligi kuu ya England katika dimba la Old Trafford pekee akiwa ni mchezaji wa pili kufanya hivyo baada ya Thierry Henry aliyefunga mabao 114 katika dimba la Highbury.

Rooney aliyocheza jana kama kiungo alifunga bao la kwanza katika ushindi wa bao 3-1 walioupata Manchester United dhidi ya AFC Bournemouth katika dimba la Old Trafford Kazi nzuri ya Antony Martial upande wa kushoto akipiga krosi na Rooney kuuweka kambani bao ambalo lilidumu mpakamapumziko.

Marcus Rashford alifunga bao la pili kabla Ashley Young hajafunga bao la Tatu dakika chache baada ya kuingia uwanjani akichuku nafasi ya Antony Martial lakini Chris Smalling alijifunga wakati akijaribu kuokoa mpira zikiwa sekunde chache mpira kumalizika.

Mechi hiyo ya jana ilikua ni ya kukamilisha. ratiba baada ya kushindwa kufanyika Juma kutokana na sababu za kiusalama.

Friday, May 6, 2016

JINSI YA KUFUZU MICHUANO YA ULAYA (UEFA NA UEROPA LEAGUE)

JINSI YA KUFUZU MICHUANO YA ULAYA (UEFA NA UEROPA)

Na Timotheo john (kwa ushirikiana na vyanzo mbalimbali vya habari)

Kuna njia kadhaa timu za uingereza zinaweza kufuzu ligi ya mabingwa ulaya pamoja na Ueropa ligi.Njia ni kama zifuatazo.

NAFASI KATIKA LIGI.
Washindi katika ligi watafuzu moja kwa moja kwenye hatua ya makundi (Leicester city wameishafuzu hatua ya makundi).washindi wa pili na tatu nao watafuzu hatua ya makundi.
Kwa timu iliyoshika nafasi ya NNE italazimika kucheza hatua ya mchujo.

BINGWA WA CL
Bingwa wa UCL Msimu huu anafuzu msimu ujao kama bingwa ntetezi.

BINGWA UEROPA LIGI
Anafuzu ligi ya mabingwa ulaya lakini kwa hatua ya awali (play off) kwa msimu ujao.

BINGWA FA CUP
Atafuzu hatua ya makundi moja kwa moja kwenye ligi ya Ueropa

BINGWA KOMBE LA LIGI (CAPITAL ONE CUP)
Anafuzu hatua ya tatu ya michuano ya Europa.

Kikomo hakuna taifa litakalotoa timu zaidi ya 5 kwenye michuano ya mabingwa ulaya (idadi ya juu ni timu 5). Huku pia timu 3 tu kutoka taifa moja zinaweza kufuzu Europa league.

JE TIMU ZIPI ZIMEISHAFUZU MICHUANO YA ULAYA MSIMU UJAO??

Leicester city wameishatwaa ubingwa wa EPL kwa maana hiyo tayari ni mojawapo ya timu itakayoshiriki UCL msimu ujao.

Manchester city wametwaa Capital one cup kwa maana hiyo tayari wameishafuzu Ueropa ligi msimu ujao katika raundi ya 3.

KWA JINSI GANI CAPITAL ONE CUP IMEATHIRI TIMU ZA EPL NA USHIRIKI WAKE MICHUANO YA ULAYA?
Mpaka sasa Manchester city wanefanikiwa kufuzu kombe la Europa katika raundi ya  3 kutokana na kutwaa ubingwa wa capital one cup.Lakini kwa sasa Manchester city wanahitaji kujilinda kupitia ligi kuu Lakini kama kuna timu itafanikiwa kumaliza nafasi ya juu katika ligi ya Epl atachukua nafasi ya Manchester city.

FA CUP INADHIATHIRI BAADHI YA TIMU?
Bingwa wa kombe la Fa anafuzu moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ya ueropa endapo alikuwa hajafuzu na amefanikiwa kutwaa kombe la Fa.

Timu kama Manchester united na Crystal palace kama zitatwaa ubingwa huu zitashiriki Ueropa league.

NINAPOSEMA KUPITIA LIGI NINA MAANA IPI??
Nina maana ya kuwa ni Muendelezo wa matukuo ya timu kutolewa.
Bingwa wa ligi (Leicester)
Tayari wameisha fuzu na wanasubiri upangaji wa kundi tu.

mshindi wa pili
Watafuzu ligi ya mabingwa ulaya.

Mshindi wa tatu
Watafuzu ligi ya mabingwa ulaya.

Mshindi wa nne
Atafuzu ligi ya mabingwa ulaya lakini ataanzia hatua ya  awali yaani Mchujo (play off)

Mshindi wa tano
Anafuzu ligi ya Ueropa katika hatua ya makundi.

Mshindi wa sita
Atafuzu michuano ya Ueropa ligi katika raundi ya tatu endapo Manchester city watamaliza. nafasi  za NNE za juu

Mshindi wa saba
Atafuzu mchuano ya Ueropa league lakini endapo Manchester united watashi taji la Fa  huku wakimaliza nafasi za sita juu huku Manchester city wakimaliza nafasi  tano za juu.

Mshindi wa Nane
Atafuzu michuano ya Ueropa league   endapo liverpool watashinda taji la Europa na wakimaliza nafasi ya saba  huku Manchester united wakitwaa Fa cup na kumaliza nafasi ya sita.huku Manchester city wakifuzu Ligi ya mabingwa ulaya.

Monday, April 25, 2016

ROONEY WA MIAKA 7 NA SASA

ROONEY WA MIAKA  7 NA SASA

Unamkumbuka Rooney wa miaka  7 iliyopita? Si huyu tena Rooney kabadilika,Hana uwezo ule tena wa miaka 7 iliyopita na kufanya awe kipenzi cha mashabiki wa Manchester united.Rooney hana jipya kwa sasa pale Manchester united lakini uwepo wake una faida kubwa klabuni hapo.

Mwaka 2002 Katika mechi kati ya Arsenal dhidi ya Everton Rooney aliifungia Everton goli la ushindi akiwa na miaka 17 siku 7 kabla ya kutimiza miaka hiyo 17.Goli hilo lilivunja rekodi ya arsenal ya kutokufungwa katika michezo 30.

Kama isingekuwa dau dogo la Newcastle huenda Rooney angetua St James park lakini Dau la £25.6 lilimpeleka katika viunga vya old Trafford ndio kwanza ana umri wa miaka 18.

Unajua kwa nini alitua Manchester united? Viongozi na mkufunzi wa Manchester united Alex Ferguson waligundua Rooney alikuwa ni mchezaji aliyekamilika.Usibishe.

Katika umri wa miaka 18 kwenye michuano ya mabingwa ulaya akifunga hat trick dhidi ya fernebahce. Utagundua alikuwa na vitu adimu.

Kwa bahati Rooney katwaa kila kitu katika ngazi ya klabu na pia katwaa tuzo nyingi binafsi kama Golden boy mwaka 2004 Kutokana na ubora wake kwa kipindi hicho

Nguvu za miguuni,Akili,Ubunifu na ujuzi ndiyo vitu ambavyo Rooney ilikuwa silaha yake na kumfanya awe na uwezo wa kufunga popote katika dimba.Bado Rooney alikuwa na uwezo wa kuwasaidia washambuliaji (Supporting forward) kutokana na uwezo wa kupiga pasi zenye ubora na kucheza kama kitimu.

Miaka ikasonga na kusonga Rooney aliendelea kuwa kioo cha mafanikio ya Manchester united kutokana na uwezo wake wa kujitolewa na kuwa kiongozi uwanjani,alifunga magoli mazuri mfano Tiki taka dhidi ya Manchester city alikuwa na miaka 26.

Ukweli unabaki pale Pale Rooney yule si huyu hana tena uwezo wa kuwasumbua mabeki,kukimbia walau hata kufunga magoli sehemu yeyote ya uwanja kutokana na uwezo wake kupungua alitumika mno enzi za ubora wake na kuvunja rekodi kadha wa kadha kwenye klabu na taifa.

Rooney hapendelei kutumika kama kiungo bado anahitaji kuvunja rekodi na kuwa mfungaji bora wa Manchester united lakini uwezo wake kwa sasa unamruhusu kutumika katika eneo moja nalo ni kiungo.

Ferguson,Moyes na hata Louis van gaal huwa walitumia na sasa lvg anamtumia kama kiungo kutokana na walijua kuwa kwa sasa Rooney anauwezo wa kukupa kitu kimoja tu miguuni mwake nazo ni pasi ndefu na fupi.pia bado kwa umri wa Rooney miaka 31 hawezi tena kucheza katika ubora ule dhidi ya mabeki wa timu pinzani anahitajika kucheza katika eneo ambalo halina presha (Kiungo).

Morgan schneiderlin, Herrera,Bastian schweinsteiger,Fellain viungo wote hao wana sifa moja kukaba lakini sio kupiga pasi za uhakika (Ndefu na fupi) ndio maana Leo De Gea huwezi kuwafunga Manchester united goli 4 wana sifa ya kuwa ni viungo wakabaji.

Tofauti kubwa ya viungo hao na Rooney ni kuwa Uwezo wa miguu ya Rooney wa kupiga pasi ndefu na fupi unamfanya Rooney alitawale eneo la kiungo.Hilo ndilo eneo pekee analoweza kucheza bila presha walau kwa miaka 3 ijayo.Ndio maana David Moyes aliishawahi kumtumia katika eneo hilo na sasa Lvg.

Majeraha na umri ni vikwazo kwa Rooney hawezi kurejea tena kwenye kilel cha mafanikio.

Si yule wa miaka 7 kwa sasa eneo pekee la Rooney ni kucheza hapo kiungo ndipo anaweza kurefusha miaka 3 ijayo katika soka lakini kuwa Mshambuliaji kwa sasa atakuwa anapoteza muda tu.

Friday, April 15, 2016

UCHAMBUZI:SERA YA MPIRA CHINA PESA INAFANYA KAZI

JICHO LANGU VIWANJANI
Timotheo john
johntimotheo6@gmail.com
SERA YA MPIRA CHINA PESA INAFANYA KAZI
Teixeira,Martinez,Ramirez,Guarin na Gervinho ni majina ambayo siyo mageni kuyasikia kutokana na Vipaji walivyonavyo lakini Pesa ikaamua iwahamishe na kwenda China kucheza mpira.Ninachokiamini Ujio wa wachezaji hao wapya unaleta taswira mpya katika soka la China.
Upende usipende kwa sasa pesa inafanya kazi kubwa katika michezo hasa kwenye Mpira wa miguu (football).wachezaji hawawezi kwenda kwenye timu kwa kuangalia ukubwa wa jina lakini maslah huenda yakaamua hatma ya mchezaji huyo.
Unapotaja mataifa tajiri huwezi kuiacha China.Wanauwezo wa kutoa pesa pesa na pesa nyingi zaidi kwa ajili ya kutimiza matakwa yao.Usibishe.Unamkumbuka Alex Texeira aliposajiliwa.kwa £ 38.7000.000 na Yule Martinez kwa dau linalokadiliwa kuwa £ 25.000.000.
Vilabu vingi kwa sasa vinavyodaiwa kuwa ni pesa vinamilikiwa na wachina (Wengine toka Asia)  huenda pesa hizo ambazo huwekezwa huko wawekezaji wakaamua kuwekeza china kwa lengo la kukuza soka la nchini humo. Sipendelei kuona pesa inafanya kazi kubwa ya kufanya wachezaji kutoa Maamuzi katika mpira. Kama wachina hawa watafika katika madaraja ya juu kisoka  watakuwa na uwezo mkubwa zaidi kisoka.
Mwaka uliopita raisi wa China alihitaji kuanza kwa haraka yafanyike mapinduzi ya kisoka nchini humo.Alihitaji kubadili muonekano wa soka la China.kauli ya kuwa mpira ni kwa watu wanaoujua haikuwa kauli hiyo tu lakini kukosekana kwa muunganiko kati ya China na Mpira pia alisema timu ya mpira hutazamwa na serikali kwa sasa ndiyo lengo lao.Kumbuka mpango wa china kwa sasa ni kuwa na academy 60000 ifikapo mwaka 2020.
Kwa sababu hizo utagundua kuwa wachina kwa sasa wameamua kuwa na mipango endelevu katika soka.Raisi anayeiongoza china amevutiwa na Mchezo wa mpira na Ndio maana sera zinawekwa ili kuangalia na kutilia suala hilo maanani.na sasa wameanza na Kutafuta players pamoja na kuhakikisha haki za matangazo ya Televisheni (Kwa sasa wapo live kupitia star times) kwa lengo la kukuza mpira wa China.
Lengo lingine litakuwa ni kutaka kuirudisha timu ya taifa ya China.Unajua kwa sasa wanawaza kwanini wazidiwe na USA??.Ndio maana kwa sasa wanahitaji ligi yenye upinzani kuliko yeyote ile ulaya.Je itawezekana kwa mizizi ya EPL au la liga??
Endapo timu ya taifa itarejea katika ubora si kwa wachezaji wajao lakini hata kwa wa sasa wanaamini " ukishinda na MTU anayefanya vyema nawe utafanya vyema kuliko yule ambaye hafanyi hivyo"lakini bado mipango yao kufikia mwakani (2017) walau kwa wiki zaidi shule 20000 ziwe na vipindi na muda wa kucheza mpira.Hii imepangwa kufanyika kwa mapana.Mpaka sasa Guangzhou wameisha jenga kituo cha watoto kwa kushirikiana na Timu ya Real Madrid na kwa sababu kuna pesa nyingi kutoka kwenye haki za matangazo ya television.Njia pekee ya soka la China kukua ni kuwekeza kwenye soka la Nchi hio.
Ninachokiamini kuwa kufikia mwaka 2020 china haitakuwa na wachezaji wakigeni tu pia hata wazawa ambao watakuwa wamejifunza vitu kutoka kwa wageni.kwa mfano.China ndiyo nchi yenye watu wengi kwa sasa nchi kama Uingereza zenye idadi ndogo ambazo hutoa wachezaji kwa nini china yenye idadi ndogo ishindwe???
Lakini lazima Wakumbuke kuwa mpira una vitu viwili cha kwanza ni sapoti na sio pesa hawataweza kufanikiwa endapo hakutakuwa na watu wa kuwatazama japo pesa wanayo.lakini pia mpira ni mchezo wa kidunia kuwa endapo mchezaji akatua Asia atasababisha na wengine na kufanya moja kati ya nchi yenye wakazi wengi kuwa na wachezaji wengi.

Sunday, April 3, 2016

PROUD HISTORY.WHAT FUTURE??

"We are having a party when a Randy learner dies" tafsiri yake ni kuwa tutakuwa na sherehe/hafla endapo Randy leaner utafariki.Hiyo ni sehemu ya mabango yaliyowahi kubebwa na mashabiki wa Aston villa.

No fight.No pride.No hope.No future mabango hayo yalibebwa katika mchezo wa Jana dhidi ya Chelsea walipofungwa goli 4-0 villa park.Proud is history.What future?? Walikuwa wakimaanisha kuyafikiria mafanikio ya kipindi cha nyuma ni kama historia na itabakia historia lakini kipi kinatarajiwa???

Kwa sasa Mashabiki wa Aston villa hawamhitaji mmiliki wa time hiyo Randolphy David leaner maarufu kama Randy leaner kutokana na nwenendo mbovu wa klabu lakini pia uongozi wake mbovu.Kumbuka Randy aliinunua Aston villa mwaka 2006 kwa dau la £62.6 million.

Wamashabiki wanapiga kelele kutokana na jinsi ambavyo Randy kashindwa kutimiza ahadi yake ya kuwekeza katika timu ya  Aston villa .Alihaidi ataifanya Aston villa kuwa tishio au kufanya mambo makubwa kama ilivyokuwa miaka 35 iliyopita ( mwaka 1980) hali ni tofauti na sasa kwani makocha na baadhi ya wachezaji wazuri wameondoka katika timu hiyo.

Martin O Neil ambaye alikuwa kocha wa Aston villa alifukuzwa kazi huku Hendrick Almstadt akiachia wadhifa mwenyewe ikumbukwe kuwa Paddy Relay wote hawa wameondoka Aston villa.Unamfahamu Remi Garde?? Katika michezo 24 alifanikiwa kushinda michezo 3 chini ya utawala wake pale Villa park.

Martin hakuweza kuleta mafanikio villa park zaidi ya kumaliza katika nafasi nzuri (lakini Leo la Randy sio hill lilikiwa ni kuhitaji kutawala soka la ulaya) katika kipindi hiki Randy alikuwa kashatumia £200m na kufikiria kuwa kumaliza bila makombe wakati umetumia pesa zote hizo tatizo litakuwa kwa kocha.

Baadaye aliletwa Brum akisema "Nilikuwa uwezo wa kushinda treble sema mashabiki hawakuwa tayari kuyapokea mafanikio yangu na Supoti.lakini baadaye alisema  "Haijalishi kocha ni yupi lakini kama hauna wachezaji hatuwezi kufanikiwa na hatujafanya hivyo" aliendelea kuwa hata wachezaji toka kwenye vituo vyetu hawapo tayari je mtafanikiweje??? Kwa hakika hii ilikuwa ni Aston Villa dhaifu.

Paul Lambert alijiuzuru si kwamba alifukuzwa ni kwa sababu ya Randy kumwambia kuwa kwa sasa hatuwezi kufanya lolote labda mwaka ujao lakini pia ukiirazama Aston villa utagundua kuwa kuondoka kwa Baadhi ya Wachezaji kama Delph na Benteke kumepelekea timu hiyo kufanya vibaya.

Aston villa msimu uliopita walifika fainali ya Kombe la Fa na kupoteza kwa goli 4-0 ndipo Delphy na Benteke wakauzwa.Kuuzwa kwa wachezaji bila kuwa na mipango endelevu na siasa kumewarudisha Aston villa nyuma na sifikirii kama Randy wakishuka atakuwa nao huenda akazidi kuwekeza Kwenye timu nyingine lakini sio kusalia Villa park tens Championship.

Ninachokiamimi Randy hana maisha marefu wakishuka hawawezi kupanda msimu ujao ni wakati wa kukumbuka histori tu ukimuona Randy mwambie hatumtaki.

Friday, April 1, 2016

UCHAMBUZI:UKIONDOKA USISAHAU ALIVYOSAHAU FERGUSON

Kuna wimbo wa mwanamama Celine Dion unasema "Goodbye is the last word I ever say", yaan "kwaheri ni neno la mwisho ninaloweza kutamka". Hakuna hisia za majonzi na maumivu makali kama pale unapolazimika kumwambia kwaheri mtu ambaye ulikwisha mzoea na kumpenda. Ni rahisi kuishi pekee yako ukiwa haujamfahamu mtu, lakini ukisha mfahamu mkashirikiana mambo mengi, mkawa karibu, sio rahis sana kumsahau na kuishi pekee yako, hasa pale ambapo utahitaji kuiziba nafasi yake. 



Utahitaji kuiziba na mtu ambaye aidha analingana na yule aliyeondoka ama anamzidi ubora , na hapo ndio huwa inakuwa mtiti. Utasikia "dah, bora hata jamaa yaan, huyu aliyepo hakuna kitu kabisa." Pata picha sasa kuwa uko na mzee wako unamuuguza, yuko hoi kitandani na unaona hawezi kupona, halafu anakwambia kwa sauti ya kukata kata "mwa.....na...ngu, so...so....gea karibu ni....ku....a....mbi....e, kuna mtaji wa Bilioni 400 nmekuhifadhia kwenye....kwenye.....eee...aah" halaf anakata roho hapo. Ni kweli utaumia kumpoteza mzazi ama mlezi lakini akili zetu wengi zitatutuma kuanza kuifuatilia billioni 400 ilipo. Unaweza hata kujikuta unalaumu kwanini hakumalizia kuongea. Kwanini asingesema mapema kabla hajakaribia zitzitahitajika






Endapo nitahitajika kutaja majina ya makocha watano bora ambao nimewahi kuwashuhudia katika ulimwengu huu, Alex Ferguson na Arsene Wenger hawatakosekana katika orodha hiyo. Kwanza historia inawabeba. Ni moja ya makocha wachache duniani walioweza kuishi na timu moja kwa miaka zaid ya 20. Lakini sio tu kuishi na timu, bali wakati huo timu zao zilikuwa katika kiwango cha juu na kuna wakati wamekuwa na viwango vya kuitetemesha dunia. Timu zikiwa chini yao hazikuwa kufutika katika ramani ya soka la ulaya. Ferguson aliingia Old Trafford mwaka 1986.



 Ameinoa Man U kwa mafanikio makubwa sana, hakuna ubishi katika hilo, ilifika kipindi miaka ya 2006 naye aliwahi kubebewa mabango ya "Ferguson Out" kuna kipindi mashabiki wa OT walihitaji yeye na Familia ya Glazer waondoke waiache timu. Yule mzee alivyo roho ngumu, hata hakushituka. Alisubiri mpaka alipoona jua limezama kabisa, akaamua kuondoka tena kwa suprise na ushindi mnono juu. Lakini alipoondoka hakuiacha Man u hivi hivi, aliwatajia mrithi wake. Tatizo langu na yeye ni kwamba hakuuambia ulimwengu wa wana Utd kitu kimoja tu. Kuwa wayasubirie mafanikio kama yake kwa muda gani.




Kama ilivyo kwa Fergie, Arsene naye ameifundisha Arsenal kwa mafanikio makubwa tu, hakuna ubishi. Kwa vipindi tofauti tofauti amekuwa akibebewa mabango ya "Arsene Out". Mzee wa watu amevumilia mengi, lakini katika kipindi ambacho naona haya maneno mawili hata yeye yamemchosha ni kipindi hiki.



 Mimi sio muumini wa wanaotamani Wenger aondoke lakini itafika kipindi tu atakubali kwenda kula pensheni. Na hapo ndipo mtiti kwa wana Arsenal utakapoanzia. Ni rahisi kuwaona makocha wazuri walioko timu nyingine, ni rahisi sana kuwatamani wanaofanya vizuri. Lakini huwa tunasahau kuwa kila kocha ana imani zake na falsafa zake. Leo hii hawa wanaopaza sauti kuwa Arsene aondoke , wanaweza kuja kuwa watoa lawama wakubwa kwa kocha atakayefuata baada ya We



nger. Wanasahau kuwa wanayemtamani atakuja kujenga kikosi anachohitaji. Kuna wachezaji vipenzi vyao wataondoka. Kuna mfumo pengine wasioutaka atauleta ,ili awapatie mafanikio kwa njia ya vikombe. Mioyo ya mashabiki wengi wa soka imekuwa mioyo ya barafu. Mimi ninaamini Wenger ataondoka Arsenal atakapotwaa kikombe cha ligi kuu, na sio mbali naamin atafanya hivyo, pengine sio msimu huu hata ujao. Na kwakuwa mashabiki tuna mioyo ya barafu, itayeyuka mara atakapofanya hivyo na hapo watahitaji abaki. Suala ni kuwa atakapoondoka atamtaja mrithi wake? Mtu wa kuishi na timu muda mrefu kwa mafanikio?

Imani yangu inanituma kuamini kuwa Wenger ni mtu sahihi kwa Arsenal japo kuna vitu vingi vinafanya leo aonekane kilaza. Hivyo vimeongelewa sana, tuviache. Suala hapa ni kuwa kama itatokea Wenger anaondoka atamuacha nani kuwa mrithi wake? Macho na masikio ya wanafamilia wa soka yatakaposikia kuwa mzee huyu anaondoka Arsenal itakuwa ni habari ya dunia nayo yataelekezwa kumsubiri yule ajaye. Je ni nani? Na hapo ndipo kwa mara nyingine busara za Wenger zitahitaj

ka. Amekuwa bingwa wa kuwatambua wachezaji wazuri, na makocha wengine wamemtumia kupata wachezaji wazuri, sasa je kwa habari ya kocha, ataweza? Atakuwa kama mzee anayekufa halafu anashndwa kutaja alipoacha billioni 400? Na kwanini hakuzitaja alipokuwa na nguvu? Fergie alitaja mrithi wake ila akasahau kuwaambia kuwa wana Utd wanahitaji uvumilivu kupata mafanikio kama aliyoyaacha yeye. 



Na  Ningeweza kumshauri Wenger ningemwambia kuwa wakati umefika kupisha Arsenal, sio kwa sababu hafai, bali, ili nao wapate kuona umuhimu wake na umuhimu wa kile wanachoita "memories" yaani kumbukumbu. Lakini Mzee hata kama utaondoka, usisahau kabisa kile alichosahau Ferguson, kuwaambia kuwa wayasubiri mafanikio kama yako kwa muda gani? Maana mzee alisahau kuwaambia Man u hilo na sasa wanatapa tapa wakifukuza makocha tu ili kuyasaka mafanikio kama ya Ferguson. Na vile ulimwengu wa sasa unahitaji mafanikio ya ghafala. Mzee usisahau kabisa.

GULINJA E. GASPER
IG & TWITTER: dc_gitaa

Wednesday, March 30, 2016

UCHAMBUZI:EGYPT WANAHITAJI POINT 1 STARS POINTS 6

Na Timotheo john

Ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Cape Verde unawafanya Morroco kuwa timu ya kwanza kufuzu Afcon mwakani.Ushindi huo unafanya Morroco kutimiza point 12 (Wamefuzu) Cape Verde 6 huku Libya na Sao tome  3.Ambapo hata wakishinda michezo iliyosaria hawatafikisha point 12 (umesalia mchezo 1)

Goli  la Ramadhani Sobhy limeitupa Nigeria nje katika Michuano hiii.Egypt ndio vijafa point  7 Nigeria 2 (Wametolewa) na Tanzania 1.Michezo miwili ya Tanzania dhidi ya Nigeria (ugenini) na ule wa Egypt (Nyumbani) itaamua Egypt au Tanzania mmoja kufuzu.

Lakini Egypt wanahitaji sare tu dhidi ya Tanzania ili waweze kufuzu huku Tanzania wakihitaji ushindi kwenye michezo yote miwili.Endapo Stars watafanikiwa kukusanya point 6 itaangaliwa Goal difference.

Goal difference
Egypt 4 v Tanzania -3
Ushindi wa 3-0 dhidi ya Stars,Sare ya 1-1 dhidi ya Nigeria na Ushindi wa 1-0 dhidi ya Nigeria unawafanya Egypt kufunga jumla ya magoli 5 na kufungwa 1 katika michuano hii.Iwa maana hiyo Mpaka sasa Egpyt wana magoli 4 ya kufunga huku wakiwa hawajaruhusu goli (kimahesabu).

Kufungwa kwa stars 3-0 na Egypt na kutoa sare ya 0-0 dhidi ya Nigeria unawafanya Stars wasife na goli lolote kwenye michuano hii huku wakiwa na hasi -3.Iki kuweka matumaini ya kufuzu Stara inatakiwa iweze kushinda goli zaidi ya 4 katika mechi 2 zilizosaria huku wasiruhusu Nyavu zao kuguswa.(Endapo stars watashinda zaidi ya goli 4 ni lazima wamfunge Nigeria na Misri kwenye hiyo michezo miwili)

Monday, March 7, 2016

UCHAMBUZI NA GULINJA::::AZAM MMELEWA POMBE YA KARIAKOO?????

Unaikumbuka ile stori ya kubuni ya mateja waliosubiri mwenzao aliyefuata kibiriti? Usijali hata kama hauikumbuki nitaisimulia kwa faida ya wengi. Mateja watatu walikuwa wakivuta bangi katika jumba moja lisiloisha(pagala), wakiwa wanaendelea na shughuli yao hiyo, wakagundua kuwa njiti zimewaishia. Hivyo wakamwagiza mwenzao mmoja ambaye naye tayari alikuwa "amesizi" akaombe kibiriti nyumba za jirani. Jamaa akatoka akaanza kuzunguka huku na huku. Akazunguka mpaka akazimaliza nyumba zote hakupata, mwisho akaingia katika jumba lile lile ambako wenzake wamo na akauza sera yake.
Jamaa: Dah, jamani samahani naomba mnisaidie kibiriti mara moja nikatumie nitarudisha. Wenzake wakajibu " Dah hata sisi kuna mshikaji tumemwagiza akatafute, kama vipi njoo tumsubiri". Kumbuka hapo anayesubiriwa ndio yule yule. Nilicheka sana siku ya kwanza ninasoma kisa hiki na nikachukulia ni mambo ya kufikirika. Kuna msemo mmoja maarufu "Chonde chonde, ulevi, nomaaa" sasa nauelewa sana. Dalili moja ya mtu kuwa katika ulevi uliopindukia ni kushindwa kujielewa na kufanya yasiyoeleweka. Naamini utakuwa umesikia na kushuhudia walevi wengi sana tangu ukiwa mtoto hadi sasa. Tofauti ni kuwa huwa wamelewa nini. Wengine ni walevi wa pombe, wengine walevi wa dawa za kulevya, wengine walevi wa kazi. Kiswahili kina maneno machache sana ya kuelezea ulevi. Kuna ulevi  wa mambo mazuri , na ulevi wa mabaya, ambao unapaswa kuepukwa kabisa. Ninachoamini ulevi ni ulevi maana kila kitu kikifanywa kwa kuzidisha ni kibaya. Mtu anaweza kuingia katika ulevi aidha kwa kushawishiwa ama kwa kuamua mwenyewe. Ukishawishiwa ni mbaya zaidi maana unakuwa huna namna ya kujimudu, na bahati mbaya sana, mara nyingi wanaoshawishiwa huwa hawawezi kuacha maana wanaowazunguka ndio watumiaji na pia hawa wanaoshawishiwa huanza na ulevi wa kiwango cha juu sana. Kama ni pombe atakunywa zile kali kali, kama ni ngono atafanya mara nyingi sana kwa wiki. Aliyeshawishiwa kuingia kwenye ulevi, huwa inakuwa ngumu sana hata kumuelimisha juu ya ubaya wa suala hilo, labda pengine mpaka waliomshawishi waanze kubadilika na  kuacha kabisa.  Kitu kinachosikitisha kwenye ulevi ni kuwa mlevi huzingatia heshima na hadhi yake pale anapokuwa hajatumia, ila atakapotumia mfano kama ni pombe, si ajabu kumkuta hata mkurugenzi fulani akiwa ndani ya mtaro wa maji machafu na hashituki kuwa yuko pabaya. Unaweza kumuona mwalimu hata kama ni profesa anajisaidia barabarani na hazingatii kuwa pengine wanafunzi wake wanamuona. Yaani ulevi hupoteza heshima ya mtu. Humgeuza mkimya kuwa mpiga kelele na pengine mpiga kelele kuwa mkimya na tatizo la ulevi humfanya kimbaumbau kuwa baunsa.

Ukiacha watoto ambao wana miaka saba hadi kumi, hapa nchini kwetu, wengine tuliobaki asilimia zaidi ya 90% ya wapenda mpira, tumekua tukizipenda timu za Simba na Yanga. Inafika kipindi hata kocha wa timu fulani ambayo nayo inacheza ligi kuu lazima awe mshabiki wa Simba au Yanga. Nakumbuka siku moja, aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa, Mecky Meksime alikuwa akihojiwa na mtangazaji wa televisheni fulani baada ya kuwa amestaafu na kukabidhiwa mikoba ya kuinoa Mtibwa Sugar. Mtangazaji akamuuliza "Wewe ni shabiki wa Yanga au Simba". Mecky akacheka kidogo na kusema kuwa yeye hana timu kati ya hizo, yeye ni mshabiki wa Mtibwa Sugar. Mtangazaji hakutaka kuamini hilo. Akandelea kusisitiza kuwa hata kama ni mshabiki wa Mtibwa lazima ana timu kati ya hizi mbili. Sikumshangaa na wala sitamlaumu mtangazaji yule kwa kuwa ndivyo alivyoamini na mara nyingi hali ilikuwa hivyo. Utawala wa Simba na Yanga ulikuwa umemeza timu nyingine nyingi kipindi kile. Hata kwenye mbio za ubingwa hizi ndio zilikuwa zinatawala, vilikuwa vibaba viwili vinapigania mke, huyu akichukua leo yule anachukua kesho. Mchezaji sijui wa Kahama United, sijui Majimaji au Ashanti akionekana mahiri tu, msimu ujao anatua Simba au Yanga. Hali hii ikapelekea hawa jamaa kujiona kuwa hakuna wa kuwazuia maana hata viongozi wa TFF/ FAT walikuwa ni wanachama wa vilabu hivi nguli( japo hili hadi leo) haikuwa inazuiliwa kiongozi kuwa mshabiki wa chama na hata leo haizuiliwi lakini pale mapenzi ya klabu yanpoongoza kuliko weledi ni kasoro(ulevi). Kwa kifupi mpira wetu wote ulikuwa Simba Yanga. Enzi hizo hata ukienda kuangalia mechi ya Taifa stars utasikia watu wanashangilia kulingana na timu zao, kumbuka timu ya taifa ilikuwa ina wachezaji wa vilabu viwili tu. Hivyo akifunga wa Yanga, mashabiki wa Yanga watashangilia, akifunga wa Simba watashangilia mashabiki wa Simba pekee yao. Hali kadhalika akiharibu mchezaji wa Yanga wa Simba watazomea na Yanga vivyo hivyo anapoharibu wa Simba. Mtu aliyemo kwenye mfumo huo wa ulevi alikuwa anashindwa kuliona hilo.

Mwaka 2008, kidogo hali ikabadilika. Azam Footbal club, walipanda daraja na kuingia ligi kuu. Mvuto wa kipekee ulijengeka maana timu hiyo kwanza ilikuwa timu ya kwanza inayomilikiwa na mtu binafsi kupanda ligi kuu. Pili ule u mwamba wa Bakhresa katika biashara ulikuwa unaleta uvuvio mpya katika soka la Tanzania, kingine ni kuwa Azam ilipanda daraja bila kucheza ligi moja misimu miwili. Yaani walicheza dara la nne msimu mmoja, la tatu msimu mmoja, la pili na la kwanza hivyo hivyo na wakapanda ligi kuu. Kwa muda pale, u simba na u yanga ulitiwa giza. Hata taswira ya timu ya taifa nayo baada ya muda mfupi ikaanza kupambwa na akina Bocco wa Azam. Nikawa najihoji sasa ikishuka daraja itakuwaje? Aah haikuwa hivyo, Azam wakawa wanapigania nafasi za juu. Azam wakanithibitisha ubora wao pale walipokuwa wanatengeneza vijana wazuri sana hasa katika eneo la kiungo. Azam ikawa tamu kama ice cream zao. Yule mzee Bakhresa akaamua kuonesha wapi tulikwama tulipokuwa tunavaa jezi za njano na kijani au nyekundu na nyeupe. Akaamua kujenga "facility" za timu pale chamazi. Uwanja wa kisasa, mabwawa ya kuogelea, gym, hostel na ofisi vyote katika sehemu moja. Akatupa sababu ya kutafuta jezi za bluu. Wakamwita Abramovic wa Tanzania. Nikawa na furaha moyoni kuwa timu zetu kubwa zitajifunza kuwa na mfumo bora zaidi wa timu za vijana, kuwa na makao makuu bora ya timu na zaidi kuwa na mfumo bora wa uongozi. Furaha ikazidi pale walipochukua ubingwa wa ligi kuu. Nikaona huu ndo mwanzo bora wa kesho nzuri. Kwa kifupi ni kuwa Azam alileta mapinduzi ya soka hapa kwetu.

Maumivuuu, hali haiko hivyo kwa sasa. Yaani tunakoelekea tunarudi kwenye zama zetu zileee. Tofauti yake tu kwa sasa ni kuwa kutakuwa na wakubwa watatu. Simba, Yanga na Azam. Kwa maana nyingine wawili wa kariakoo ama wakongwe na mmoja wa Chamazi. Wakongwe ni wazoefu katika masuala ya ujanja ujanja katika ligi. Wanajipangia marefa, wanarubuni wachezaji wa timu pinzani ama walioko nje ya nchi, wanarubuni makocha, hawakosi sababu kila wanapofungwa na mara nyingi sababu zao lazima mtu alaumiwe. Azam naye amekwisha kinywea kikombe cha wakongwe wa Kariakoo. Sasa hivi utasikia Azam anahusishwa na skendo ya kupanga marefa, anatoa sababu za lawama pale anapopoteza mchezo, anapata safari ya kwenda nje katikati ya ligi kucheza bonanza anakwenda, hataki kuuza wachezaji wa kiTanzania nje ya nchi kwa kuwarubuni kimtindo. Hahaha yaani tumekaa tunasubiri jamaa akalete kibiriti na mleta kibiriti naye amekaa anasubiri. Ulevi nomaa. Kwa waliyokuwa wameyafanya Azam nilitegemea wangeendelea kuwa mfano na kuwaburuza wakongwe katika mpira huu, kuanzia kiuongozi hadi kimchezo na kimataifa lakini wamekwama nao. Juzi katika mechi ya Azam na Panone namsikia kocha wa Azam anasema "This is a pitch for goats" yaani " Huu ni uwanja wa mbuzi" sio uwanja wa kucheza binadamu wanapaswa kucheza mbuzi. Kidogo niliona ni sababu ya maneno. Uwanja wa ushirika naamin ni maoni ya kwanza kusikia ukisemwa ni uwanja wa mbuzi. Azam wameangukia kwenye mtego ule ule wa wakongwe, nao wanahusishwa na dili za upangaji wa ratiba, upangaji wa marefa na kuhujumu wachezaji. Hadi sasa tunapoongea sijasikia Azam wakiuza mchezaji kwenda nje ya nchi, hasa MTanzania. Cha zaidi ambacho nimepata kusikia ni skendo kuwa waliwarubuni baadhi ya wachezaji waliopata nafasi ya kufanya majaribio ulaya ama nje ya Tanzania kwa kuwapa magari mazuri, kuwaongezea mishahara na kuwawekea vizuizi vya kiuongozi. Sio mabaya kuwalipa vizuri wachezaji lakini kwa maslahi ya Taifa mchezaji anahitaji kupata jukwaa bora zaidi kwa ajili ya kuongeza kiwango, tofauti na ligi ya hapa ndani. Maana kama Azam angekuwa na uwezo wa kuwatumia vyema wachezaji hawa angalau angethibitisha kwa kufika mbali michezo ya kimataifa. Siku baada ya siku Azam inazidi kuwa ya "Kitanzania", sio ya kisasa tena.

Bado hamjachelewa, mnisamehe kama nakosea, lakini ninapenda nishuhudie mapinduzi ya kisoka na mwanga wa hilo hapa nchini, mnao ninyi. Mmekuwa wa kwanza kwenye mambo mengi sana. Iko wapi furaha mliyonipa kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu? Yako wapi matarajio makubwa mliyoniandaa kuyapokea pale mlipojenga uwanja wenu Chamazi? Uwanja ambao hata hivyo hamjawahi kuutumia kwa mechi za Simba na Yanga. Uko wapi mshangao mlionipa kwa kuwapa nyumba wachezaji wenu wote? Ziko wapi sifa nilizowapa kwa kuleta basi la kisasa la wachezaji? Ulimwegu wa wanasoka unatamani kuendelea kushuhudia mambo makubwa kutoka kwenu. Cha ajabu ni haya madoa ambayo mnapakwa na matukio ambayo yanawafanya muonekane kufanana na wakongwe. Ndio, wakongwe wale wa Kariakoo. Mmoja msimbazi mwingine Jangwani. Wale ndio tumezoea kuona wakihusishwa na migogoro na skendo za kila aina kila wakati. Mwaka huu Simba wakitulia, ujue Yanga kutazuka tatizo, Yanga nao wakitulia linaibukia msimbazi mpaka ninaamini kuwa kule kuna pombe ya aina moja wanayoitumia, naam, pombe ya Kariakoo. Cha kuzingatia sana ni kuwa ukimwamsha aliyelala utalala wewe, simba wamefungua duka rasmi la vifaa na bidhaa za timu, mbeya City wana bidhaa za timu kila kona lakini ninyi waamshaji mnarudi kule. Kwa uongozi wa Azam ulivyo sikutegemea haya yatokee. Na hapo ndio ninapatwa na wasi wasi hadi najiuliza, Azam, mmelewa pombe ya Kariakoo??

GULINJA EZEKIEL GASPER
IG & TWITTER: dc_gitaa
Whatsapp: 0766562588

©Gitaa Inc.

Sunday, March 6, 2016

UFAFANUZI KUHUSU SHERIA NAMBA 11 YA OFFSIDE

Na Timotheo s john

NAFASI YA KUOTEA . Tunapozungumzia
nafasi ya kuotea tunaangalia vitu vitatu
yaani:
1. Mshambuliaji
2. Mpira,
3. Mlinzi.

KUJIHUSISHA NA MCHEZO.
1. Kujihusisha na mchezo
2. Eneo ambalo mchezo unachezwa
- Kwa Kuingilia mchezo
- Kwa Kumuingilia mpinzani
- Kwa Kupata faida baada ya
kuwepo kwenye nafasi ya kuotea.
Tafsiri ya sheria hii inasema ya kwamba,
Sio kosa kwa mchezaji kuwepo katika
nafasi ya kuotea; na mchezaji atakuwa
kwenye nafasi ya kuotea endapo atakuwa
karibu zaidi na mstari wa goli la timu
pinzani kuliko VYOTE yaani Mpira na
Mpinzani wa pili wa mwisho.
Mchezaji atakuwa hayupo katika nafasi ya
kuotea endapo;
· Atakuwa amesimama kwenye nusu
yake ya kiwanja cha mchezo
· Atakuwa amesimama sambamba na
mpinzani wa pili wa mwisho.
· Atakuwa amesimama sambamba na
wapinzani wawili wa mwisho.

KOSA LA KUOTEA.
Mchezaji aliyesimama kwenye nafasi ya
kuotea ataadhibiwa kwa kosa la kuotea
endapo wakati mpira umechezwa au
kuguswa na mchezaji wa timu yake,
mchezaji huyo kwa maoni ya mwamuzi
atajihusisha kucheza kwa:
· Kuingilia mchezo
· Kumuingilia mpinzani
· Kupata faida baada ya kuwepo kwenye
nafasi ya kuotea.

SIO KOSA.
Sio kosa endapo mchezaji atapokea mpira
moja kwa moja kutokana na:
· pigo la Goli
· pigo la Kona
· Au Mpira wa kurusha

Monday, February 29, 2016

UCHAMBUZI:RASHFORD JIFICHE KAMERA ZISIKUMULIKE

RASHFORD JIFICHE, KAMERA ISIKUMULIKE.

Ninacheeeka sana, nina furaha na amani moyoni, sio kwa ajili ya ushindi wa Man U dhidi ya Arsenal, nimekumbuka enzi zangu za utoto. Miaka takribani 15-19 iliyopita, nilikuwa mtoto, mtoto wa maajabu naweza kujiita. Nadhani ndio nililelewa hivyo na wazazi wangu, kuwa kila kitu ninachoona nikakipenda  basi ninaweza kukifanya, tena kwa ufanisi. Nilikuwa nina juhudi ya kujua kila kilicho bora. Ilikuwa sio ajabu ukinikuta ninawasimulia watoto wenzangu habari za siasa za magharibi kipindi cha vita baridi, wala haikushangaza kunikuta nikiwafundisha hata watoto wa kiisalamu habari za Yesu kristo, sasa habari ya mpira na kuwajua wachezaji wa ulaya nadhani mtaani kwetu na hata shuleni nilikuwa na wapinzani wachache sana ambao mpaka leo nawakumbuka kwa majina. Lakini pamoja na ujuvi huu nilikuwa siwezi kuishinda aibu na uoga. Nilikuwa najificha mbele ya wageni na hata inaponilazimu kukaa mbele yao nilikuwa mkimya sana. Baba yangu, wakati huo, alinipenda na akanitumia vzuri kama nishani ya kung'aza sifa za familia. "Aah ka kijana kangu haka, ka G, kanajua wachezaji woote wa dunia nzima" ilikuwa kauli maarufu pale stori zinapopamba moto baina ya mzee na marafiki zake, wakati mwingine " ka G kanatengeneza vifaa vya umeme, iwe TV, rimoti hata pasi". Nilijisikia fahari sana, ila mshangao mara nyingi ulizikumba nyuso za wasimuliwaji. Hawakuweza kuoanisha kati ya udogo wangu na makubwa yanayonenwa, jambo ambalo lilinifanya kuwaduwaza pale ninapopewa nafasi ya kuthibitisha maneno ya baba. Nilikuwa katoto kapenda sifa ambako hakajioneshi, kanasubiri kuwaduwaza watu.


Jina ambalo limepata umaarufu wa ghafla kuanzia Carrington, AON complex mpaka Old trafford wiki hii ni, Marcus Rashford. Sio mengi sana tunaweza kuyajua kuhusu huyu kijana. Alizaliwa tarehe 31 mwezi wa 10 mwaka 1997 (anazidiana miezi miwili tu na mdogo wangu anayenifuata). Mtoto huyu alianza kucheza mechi yake ya kwanza kwenye kombe la FA la vijana dhidi ya Leicester mwaka 2014. Aliwashangaza walimu wake Paul McGuiness ambaye alisema ana kipaji cha aina yake na Warren Joyce ambaye aliamua kuanza kumtumia kama mshambuliaji wa mwisho katika kikosi cha vijana baada ya Mitchell kuumia na huyu dogo akaweza kuwa mfungaji bora wa msimu wa 2014/2015. Kwa mara ya kwanza ameingia uwanjani katika kikosi cha wakubwa kwenye mechi ya Europa dhidi ya Midtyjlland na kufunga goli mbili. Mshangao ni kuwa, alikuwa mtu wa mwisho kabisa kutajwa katika kikosi cha siku hiyo baada ya Anthony Martial kuumia mazoezini siku hiyo, lakini pamoja na hayo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga katika michuano ya ulaya. Jana dhidi ya Arsenal ameorodhesha jina lake kwenye orodha ya wachezaji wadogo waliowahi kuifungia United katika ligi kuu, yeye ni wa tatu baada ya Macheda na Welbeck. Nikimtazama Rashford, tangu katika mechi ya Europa ninaona washambuliaji fulani fulani ndani yake. Ninaweza kumuona Macheda ndani yake, ninamuona Berbatov ndani yake, na endapo atafanikiwa kuwa na msuli zaidi ya sasa anaweza kuwa Drogba. Sikupanga kumtilia maanani sana lakini vitendo vyake vya ujasiri mbele ya beki za Arsenal vimenivutia zaidi, kwa mtoto mdogo vile kuwa na ujasiri wa kutaka kukatiza katikati ya Bellerin na Paulista ama kutaka kukimbizana na Koscielny, ama kuweza kujiweka katika nafasi nzuri za kupokea krosi mbele ya ukuta wa Arsenal ni jambo la kustaajabisha. Hata hivyo ninakumbwa na wasi wasi kama alionao kocha wa Man U, Louis Van Gaal kwamba hawa vijana huweza kufanya vizuri mechi ya kwanza lakini suala ni mechi ya pili na ya tatu hadi ya nne na kuendelea, je, ataweza kuendeleza huu ubabe? Ataendelea kukua na kukomaa? Ni muda pekee ulioficha siri hii.

Kwa siku za karibuni, wameibuka vijana wenye vipaji vya aina yake. Wengine tukawafananisha na majina makubwa yaliyowahi kutokea katika soka. Tulitegemea makubwa kwao lakini wengine, tena wengi walituangusha. Wengi wamepotea. Wamekuwa wa kawaida sana na pengine wamekuwa wabovu. Inatunyima imani sana sasa kuwategemea sana watoto wadogo wenye kuonesha ishara nzuri. Moja ya vitu vinavyochangia sana hili ni vyombo vya habari. Vyombo vya habari viko macho sana kutafuta habari kuliko kuweka ukweli. Vinaishi kwa matukio kuliko uhalisia. Vyombo vya habari yaani magazeti, televisheni, redio na mitandao vinaweza kukufanya uishi maisha ambayo huyataki, vinaweza kukufanya ujaribu sana kuishi wanavyotaka na hapo ndio ugomvi wao na LVG, Mourinho na Ronaldo unapoanzia. Wanakuzonga, wanakukosesha raha. Lakini hili hunoga zaidi kwao unapoamua kuishi mbele ya kamera zao. Depay, Sterling, Januzaj, Walcott na wengine wengi ni wahanga sana wa suala hili. Utagundua kuwa hili tatizo liko uingereza sana. Anthony Martial amejificha, kamera zilimmulika mwanzoni lakini akajua jinsi ya kuishi nazo, hivi sasa hakuna ubishi kuwa Martial ni mchezaji muhimu Utd japokuwa hakustahili kuvaa majukumu hayo mapema hivi. Akina Messi na Neymar wamejifunza namna ya kuishi nyuma na sio mbele ya kamera, haziwasumbui tena. Ugonjwa bado uko uingereza.

Moyoni mwamgu natamani sana Rashford lije kuwa jina linalotamkwa sana huko baadae, natamani aje kuwa Van Nisterooy ama Rooney wa zamani yule ambaye mpaka sasa anaheshimiwa kwa matendo ya kale. Haya yanawezekana tu endapo atawekwa chini ya uangalizi wa watu wazima, asibebeshwe majukumu makubwa asiwekwe kila wakati. Ifike kipindi mashabiki wamtamani awepo na kila akiingia anatuachia cha kujadili mpaka atakaporudi. Ndio maana ninacheka, maana natamani Rashford awe kama 'ka G', mkimya, mwemye aibu mbele za watu, awe sifa mbele ya baba yake LVG, ili baba yake aweze kumtumia kama fimbo ya kuwaumiza adui zake. Cha kuchekesha ni kuwa Rashford hajawahi kuniona, na hajawahi kunisikia hata pengine wakati 'ka G' kanahangaika kung'arisha jina mbele ya wageni wa mzee yeye alikuwa ananyonya. Wakati huo nina ndoto za kuwa rubani na yeye hatambui kama ana mguu wa mpira. Lakini ni vyema sana akawa tu hivyo kama, itamjengea sana jina kubwa baadae. Ombi kwa meneja ni kwamba asimpange sana huyu dogo maana hata jeraha la Martial sio la muda mrefu. Rashford abaki kuwa "suprise package" hapaswi kabisa kuvipa mianya vyombo vya habari kuhangaika naye. Ni kweli anahitaji uzoefu zaidi, lakini huu ndio wakati ambao historia za akina Ronaldo, Messi, Xavi na Welbeck zinahitajika zaidi. Wengine pia ambao wanaweza kutumika kama "bad examples" wasisahaulike. Rashford ama Rashid kama anavyoitwa vibanda umiza anapaswa kuendelea kulelewa tu.


Wakati huu ni vigumu sana kwa Man u kuukubali ukweli huu maana watoto hawa ndio pekee waliopo. Na Timu inahitaji kushinda. Lakini kwa manufaa ya baadae mechi chache zijazo zinapaswa kumlea Rashford kuliko kumpa majukumu. Falsafa ya LVG inapenda sana kutengeneza vikosi vya baadae, lakini kwa maisha ya uingereza, sio vyema sana kuishi mbele ya vyombo vya habari. Uingereza na Tanzania ni kama tuna tamaduni zinafanana. Tunapenda kusema mambo kwa kuyakuza sana bila kujali athari zake kwa wasemwaji. Ndio maana huwa najivunia sana maisha ya 'ka G' maana kalipenda siku zote kuushangaza ulimwengu. Kukiweka katika namna ambayo hakuna mtu hutegemea kanachoweza kutenda. Ni kama tu kuishi nyuma ya mlango wakati unaujasiri wa kuonekana. Ningepata nafasi ya kuongea na mdogo wangu Marcus Rasford ningemsihi ajifiche, nyuma ya mlango, ili kamera za waingereza zisipate kummulika na kumfanya aishi maisha ambayo yeye hajayatamani. Nilifurahishwa na jibu lake, kwamba hatasherehekea ushindi maana leo ana mtihani wa Kemia, safi sana dogo. Hivyo hivyo, usiwe kama msanii wa bongo flava aina fulani fulani, ukitoa ngoma moja ikapigwa Kenya unanunua gari na kuanza starehe kisha unasahau kazi za studio. Piga kitabu, piga mpira, piga magoli lakini usisahau kabisa kuwa unapaswa ujifiche, kamera isikumulike.

~GULINJA E. GASPER~
IG & twitter :dc_gitaa


Monday, February 15, 2016

UCHAMBUZI::::MACHO ULAYA MASIKIO CHINA

Na Gulinja Ezekiel Gasper

Umewahi kuona mtu anaangalia Tv huku anasikiliza redio? Hapo utakuta sauti ya Tv iko chini sana. Hii ina maana kuwa anapenda kutazama kinachooneshwa lakini pia hataki kupitwa na kinachotangazwa redioni. Bahati mbaya ni kwamba hauwezi kuwa unasoma gazeti, unaangalia Tv na kusikiliza redio kwa wakati mmoja kwasababu njia za fahamu zitumikazo hapo ni mbili tu, macho na masikio. Kwahiyo ili uelewe unapaswa aidha kuzingatia kimoja ama viwili huku ukigawa majukumu kwa masikio kusikiliza na macho kuona. Zamani tulikuwa tukipata taabu sana kuweza kugawanya majukumu ya milango hii ya fahamu hasa katika masuala ya mpira. Ulikuwa unalazimika aidha kwenda uwanjani kuangalia ama kusikiliza kwenye redio. Ilikuwa ni nadra sana kufanikisha viwili hivi kwa pamoja. Lakini kwa jinsi teknolojia ilivyokua hata ligi kuu ya Tanzania unaweza kuitazama huku unasikiliza muziki redioni.

Unatambua kuwa ligi kuu ya China ina umri wa miaka 12 tu? Eeeh hii hii inayoitwa China Super League(CSL) kabla ya 2004 walikuwa na ligi daraja la kwanza tu. Katika kipindi kama hiki jamaa wameifanya ligi kusimama, usiniambie kuwa ni suala la utandawazi wakati kwetu, ligi ina umri mkubwa kuliko mimi na utandawazi haujaivusha. Siku zote nimekuwa muumini wa "opportunists" waviziaji ama watu wanaotumia fursa vyema. Turudi kwenye CSL. Ligi hii ina jumla ya timu 16 (kama ligi ya Tanzania). Mtindo wa kushuka na kupanda daraja ni timu mbilimbili. Kama ilivyo uingereza CSL ina ligi ya timu za akiba lakini cha kufurahisha ni kuwa, kila timu iliyoko ligi kuu ina timu ya U20, U17 na U15, ambazo nazo hucheza ligi yake.  Ligi hii huanza mwez wa pili au wa tatu na kuisha mwezi wa kumi na moja au wa kumi na mbili. Timu saba tu zimekwisha shinda ligi hii huku Guanghzou Evergrande ikiongoza kwa kubeba mara tano.

Yatakuwepo mengi sana uyajuayo kuhusu ligi hii ya China, pengine kwa kusoma ama kusikia. Ninachotaka tuzingatie leo ni maajaby yanayotendeka nje ya viwanja vyake, yaani katika ofisi za timu. Ligi nyingi za nje ya ulaya zimekuwa ni vyanzo vya kuzalisha vipaji vchanga(mfano ligi za Brazil na Argentina) ama zimekuwa zikipokea vipaji vilivyochoka ulaya. Wataalamu wa mambo husema watu huenda kula pensheni huko (mfano ligi ya Marekani na Uarabuni). Hata ligi ya China ilipoanza kuwanunua akina Anelka na Drogba tuliichukulia ni "ligi ya pensheni" lakini nionavyo sasa hilo si kweli tena. Kilichonishtua mimi ni mkataba wa TV walioupata hawa jamaa billion nane dola za Kimarekani!!!! Inashangaza iliyoje, hata Eredivise hawajafika.

Kinachonifurahisha katika ligi hii ni kuwa mambo haya sio ya kupita tu. Rais wa nchi, ndiye ameshikia bango suala hili. Ndiye ameainisha uanzishwaji wa sera bora ya mpira wa miguu nchini humo. Wachina ni watu wa kutazama, kupenda na kuamua. Wakiamua jambo lao linakuwa. Walipoamua kutengeneza nakala za vifaa vya kielektroniki vya makampuni makubwa wakaweza, walipoamua kuwekeza Afrika, mzungu amewapisha. Kwasasa China ndio nchi inayoongoza kwa uwekezaji na kufanya biashara Afrika. Kwa lugha nyingine ndio wanaoongoza kwa umiliki wa rasilimali duniani maana Afrika ina rasilimali za kutosha sana. Sasa hizi pesa wanazozitoa kwetu huku ambazo kila siku tunawapelekea zinawekwa wapi kule kwao? Ubunifu wao umeingia katika soka.

Tofauti na inavyoaminiwa sana kuwa waChina ni watu wa vitu rahisi kwa bei rahisi, kwenye mpira wameingia na gia nyingine. Ni kama wamekuja kupambana na vilabu vya ulaya. Wengi tusingeshangaa kununuliwa kwa Drogba au Anelka kule lakini kwa habari ya Texeira, Ramirez, Jackson Martinez, Gervinho mhh. Wako serious. Kumbuka huko kuna Robinho, Asamoah Gyan na kocha kama Scolari. Asubuhi nikipita mitandaoni ninakutana na habari kuwa Rooney, Obafemi Martins na Ezequiel Lavezzi wanahitajika huko nikatabasamu tu. Kwa kasi hii hawashindwi kumshawishi Mata ambaye Mourinho hamtaki pale Utd na si muda mrefu watapiga hodi kwa Akina Coutinho, Herera, Ox na wengine. Kwa Remy wameshafika sasa cha kufurahisha ni kuwa wameweka hata dau kwa Messi.

Kinachonifurahisha mimi sio hizo bei zao bali ni kuwa tunapata sehemu nyingine ya kusikiliza mambo mpira, lakini kizuri zaidi ni kuwa hawa wataalamu wanaonunuliwa huko hawaendi kula pensheni tu, wanakwenda kuwapa motisha vijana wa umri wa chini ya miaka 20 ambao wanacheza kule. Ni funzo zuri toka kwa wachina. Ni kweli hatuna rasilimali pesa lakini kwanini tusipate sera nzuri ya michezo? Wachina wametupita kuanzia teknolojia na sasa wanaenda 'kutuzidi sana' kwenye mpira. Kuna timu zina uwezo wa kumiliki shule za mpira wa miguu lakini zinasubiri mpaka 'club licencing' ya CAF iseme kuwa ni lazima kumiliki timu za vijana. Hata hivyo bado hakuna sera nzuri kwa soka la vijana ambayo hata hizi timu chache zenye timu za vijana zinapaswa kuitumia. Sisemi kuwa na sisi tuanze kuwanunua akina Abou Diaby kuja kuwapa motisha wadogo zetu, la hasha, hatuna uwezo huo lakini je, uwezo wetu umeishia hapa?

Bw. Malinzi alipokuwa akigombea urais wa TFF nilimfurahia na kuona ni tumaini jipya kwa soka la vijana, sijui amefika TFF akanywa maji yaliyowalevya akina Rage naye akasinzia au amenogewa na utamu wa mgawo. Kajitahidi kuwa nchi yetu itaandaa fainali za U17 mwaka 2019 lakini akasahau kuwa tunahitaji maandalizi ya kudumu sio ya u17 fainal za afrika tu. Magufuli wa hapa kwetu anaweza asiwe na kipaumbele kama Magufuli wa China(Rais Xi), je Malinzi wa hapa kwetu hawezi kufanya kitu angalau tukawa tu na kanuni zenye kulazimu ligi iwe na timu za vijana? Au suala ni udhamini? Kama ni hvyo ichezwe ki kanda tu kama ligi daraja la kwanza.

Kiukweli nmechoshwa na timu  kufungwa michuano ya kimataifa halafu sababu ikawa uzoefu. Tutautoa wapi uziefu ikiwa mtu anatoka kucheza ndondo anaenda ligi kuu? Tunategemea zali la Vardy? Uzoefu tutaupataje ikiwa mtu wa miaka 24 aliyeko mtaanindo kwanza anawaza namna ya kucheza afike daraja la tatu. Anyway nisiumize sana kichwa kuhusu mpira wa Tanzania yangu maana najua Samatta atabaki Samatta, na sisi ni wawindaji wa vipaji maana hatutambui kuwa jua la mawio na machweo yanafanana lakini sio sawa, tuko bize kuangalia ujuzi wa Messi na Ronaldo na kusikiliza dau wanaloweka waChina. Sio mbaya maana kwa sasa macho yako Ulaya na masikio yetu yako China kuja kutahamaki wao mbele sisi nyuma.

GULINJA E. GASPER

Tuesday, February 9, 2016

UCHAMBUZI.NAKALA NA HINJO

NINACHOAMINI MAESTRO
NI PALE TAJIRI ABRAMOVICH ALIVYOMLETA
PEP GUARDIOLA KWA TAJIRI WA KIARABU.
Na: Ayoub Hinjo
E-mail: hinjo38@gmail.com
Simu:0787624009/0719772772
Ndugu msomaji,ukishindwa kujiandaa basi
jiandae kushindwa. Mafanikio siku zote hayaji
tu ukiwa haujishughulishi kwa juhudi. Sasa
jaribu kuifikiria Chelsea ambayo ilikuwa haipo
chini ya tajiri wa Kirusi ilikuwa timu ya daraja
la kati. Ilikuwa timu yenye kutoa ushindani wa
hali ya juu kwa timu za daraja la juu kama
ilivyo kwa Leicester City kwa sasa,Newcastle,
Everton,Blackburn,Tottenhamna nyingine nyingi
ambazo zilizotoa ushindani wa hali ya juu na
kutwaa ubingwa dhidi ya vigogo. Sasa Chelsea
ni timu ya daraja la juu. Timu iliyojipatia
mashabiki wengi kuanzia pale alipoanza
kuimiliki Roman Abramovich. Chelsea
wamebadilika na tangu hapo imepitia kwa
makocha wa hadhi yao sasa.
Chelsea ni miongoni mwa timu kutoka
Uingereza zilizoshinda karibu kila kombe
walilopigania. Wameshinda Ligi kuu,FA,Capital
One,UEFA Europa cup na UEFA Champions
league cup. Katika makombe yote ambayo
wameshinda Chelsea hakuna lenye thamani
kubwa na lenye heshima zaidi ya UEFA
Champions League,hili ni kombe la mabingwa
wa Ulaya. Kombe linaloshirikisha timu zenye
hadhi kubwa na zenye mashabiki wengi
duniani. Kwa kifupi ni kombe la wanaume
matajiri. Abramovich alikuwa na hamu ya
kushinda kombe hilo pamoja na uwekezaji
anaofanya Chelsea anatamani kushinda tena
na tena kombe hilo na bado anatamani kuona
timu yake inaendelea kushiriki zaidi na zaidi
kwenye michuano hiyo. Ni michuano ambayo
kila hatua unayosonga unapata pesa za
kutosha. Hii ni michuano inayofanya timu za
Uingereza zigombanie nafasi 4 za juu hili
zipate kushiriki. Si ligi ya Uingereza tu na ligi
nyingine zinapigana vikumbo kupata nafasi ya
kushiriki na kushinda kombe hilo lenye thamani
kubwa.
Manchester City itakuwa chini ya Pep Guardiola
kuanzia msimu wa 2016/17 sasa ni muda wao
wa kubeba kombe na sio kushiriki tena.
Matajiri wa Kiarabu wamewekeza pesa za
kutosha na wanazidi kufanya hivyo. Kama
ilivyokuwa kwa Chelsea sasa wanaamini ni
muda wao kuiteka dunia. Ni muda wao kupata
wanachostahili kutokana na uwekezaji
wanaoufanya. Kwa uwekezaji wanaofanya
halafu usishinde kombe lenye hadhi ya UEFA ni
sawa na bure kabisa na hiyo ndio sababu
kubwa ya kumpa kazi Pep Guardiola. Kocha
ambaye ameshinda kombe hilo mara mbili na
ni kocha ambaye karibu kila mchezaji
anapenda kupata mafanikio chini yake.
Kumpata mtu kama Guardiola ni rahisi kwa
Manchester City kupata wachezaji wenye hadhi
ya juu na wenye kuwafikisha kwenye mafanikio
wanayoyataka. Inawezekana kumpata Pep
kutaifanya Man City wapate mafanikio kuanzia
kibiashara zaidi sababu wawekezaji wengi
wanapenda kuweka pesa zao sehemu salama
na yenye kuleta mafanikio kwao na kuipeleka
kuwa miongoni mwa timu moja tajiri zaidi.
Kuwa na Pep ni zaidi ya faida kwao kibiashara.
Naamini kumkosa Pep Guardiola matajiri hao
wangekula sahani moja na Jorge Mendez
awaletee Mourinho ambaye hana tofauti sana
na Guardiola zaidi ya soka lake linaloboa.
Naamini matajiri wa Kiarabu hakuna zaidi
wanachokitaka sasa zaidi ya kombe la UEFA
Champions League,wamechoka kushiriki.
Kufikia mafanikio ya Manchester United
inaweza kuwachukua muda zaidi ila kupata
kombe kubwa linaloshindanisha timu kubwa
itakuwa ni kitu cha kipekee zaidi kwenye
historia yao. Sishangai kuona Perez wa Real
Madrid anavyoangaika kila kukicha kuleta
wachezaji wenye hadhi ya juu zaidi duniani hii
inatokana na kuhitaji UEFA na kuvutia
kibiashara zaidi kwa wawekezaji. Ilikuwa ni
matusi makubwa kwao kama wengeshindwa
kushinda kombe la UEFA Champions League
dhidi ya Atletico Madrid sababu uwekezaji wao
ulikuwa ni mara 10 zaidi ya wapinzani wao.
Asante Abromovich kwa kumleta Pep Guardiola
kuwa mtumishi wa Matajiri wa Kiarabu kutoka
Abu Dhabi.

UCHAMBUZI.JUA LA MAWIO NA MACHWEO HUFANANA TUTAZAME MASHARIKI

Umewahi kujiuliza kuwa endapo utapoteza fahamu ikiwa ndio kwanza jua linachomoza (kwa watu wa magharibi watanielewa zaidi) kisha ukazinduka jioni wakati jua linaelekea kuzama, nini kitatokea? Unaweza kudhani kuwa muda haujakwenda tangu ulipopoteza fahamu, mpaka akili itakapotulia na ukatambua mashariki ni wapi na magharibi ni wapi. Miaka kadhaa iliyopita mimi na familia yetu tulisafiri kwenda kwenye maziko ya marehemu mama mkubwa (mama yake babu yangu), maeneo ya mcharo wilaya ya bunda. Baada ya shughuli ile, asubuhi iliyofuata tulifanya safari kwenda kijiji kingine kumsalimu dada wa marehemu, nakumbuka vyema kuwa nilikuwa mgonjwa kiasi wakati ule. Nilikuwa nafurahia zaidi mwangaza ule wa jua la asubuhi unavyoonekana katikati ya majani marefu upande wa mashariki. Usingizi ulinipitia na nilipokuja kushtuka tulikuwa tumekwisha fika na niliamshwa kwa ajili ya chakula. Macho yangu haraka nikayakimbiza kwenye jua na nikaona rangi ile inayonivutia ikiwa inaangaza, sikushituka mpaka niliposikia mtu akisema kuwa ni saa 11 jioni na hapo ndipo nilitambua jua limekwenda magharibi haliko tena mashariki.

Japo jua la mawio na machweo yote hutupatia Vitamin D lakin yana tofauti kubwa. Unapoona jua la mawio ni dalili kuwa unaanza siku mpya na unao wakati wa kuyatengeneza mafanikio yako ya siku hiyo na pengine ya baadae, hapa ndipo tunapozidiana ujanja, katika matumizi ya huu muda tuliopewa. Eneo hili la matumizi ya fursa ndio linamtofautisha Messi na Sadio Mane, hapa utaiona tofauti kati ya Chicharito na Sturridge. Kila kiumbe kimepewa masaa 24 ya kuishi kila siku, ni kama tumepewa mtaji wa kuanzia ni wewe unaamua uwekeze wapi, kwenye biashara ya nyanya ili uingize kidogo kidogo utengeneze mtaji wa biashara ya magari au unaamua kuwekeza kwenye vyote viwili kwa mtaji mdogo ulionao na unaamini kuwa utaweza kuvimudu. Matokeo ya kuwekeza katika vyote viwili ni kuwa biashara hizo zitakufa moja baada ya nyingine na utaanza tena kutengeneza mtaji wa kuanza biashara nyingine. Hii nyingine nayo bila mkakati madhubuti itakufia mikononi.

2019 inaweza kuonekana mbali sana kwa matamshi lakini ki mahesabu imeshafika na iko mlangoni. Ninapouwaza mwaka 2019 moja kwa moja kwenye akili yangu linakuja neno U17 (under 17), labda ni kwakuwa sijawahi kushuhudia nchi yangu ikiaandaa michuano mikubwa ya soka zaidi ya CECAFA SENIOR CHALLENGE, au ni kwakuwa sijaona timu yangu ikishiriki fainali za michuano mikubwa zaidi ya CHAN, ambayo nayo tuliishia raundi ya kwanza. Naisubiri kwa hamu 2019 ili niweze kushuhudia yote hayo mawili yakitukia kwa pamoja. Lakini swali ni je, tutafika wapi kaka wenyeji? Je, huu utakuwa ni mwanzo wa sisi kwenda kucheza fainali za kombe la dunia? Ama itakuwa ni bonanza? Je, itakuwa ni njia ya kuelekea kushuhudia majina ya wachezaji wa nchi yangu kwenye nyuz nyeupe za Real Madrid ama yatabaki kwenye nyuzi za Azam, Simba , Yanga na pengine Mwadui?

Wakati nikitafakari haya najiuliza kuna mkakati mkubwa unaoonekana wa kujiandaa na haya? Kuna Jua la mawio na jua la machweo, sijui ni kwasababu tulipoteza fahamu na tumezinduka tukakuta yote yako angani sasa tunashindwa kutambua lipi ni lipi kwa kuwa yanafanana rangi! Ingekuwa ni amri yangu ningeomba kuipumzisha kwanza Taifa stars kushiriki mashindano ya kimataifa ama kama hilo sio bora basi ningeiacha iendelee na utaratibu huo lakini nguvu yangu kubwa nikaielekeza kwa timu ya U13 ambayo niliishuhudia Morogoro na mara ya mwisho niliisikia iko Tanga, ukiniuliza ilipo leo sifahamu. Hili ndio jua letu la mawio, huku ndio kuna samaki wabichi tunaoweza kuwakunja. Hawa wengine wa jua la mawio hata tukiwakunja mkia utabaki nje tu, mwisho wa siku wapita njia watawavuta nje ya chombo kama ilivyozeleka. Ni ajabu sana kuona wanaopaswa kutushika mkono na kututazamisha mashariki nao  wanatazama magharibi na wengine bado hawajazinduka kabisa. Nani wa kumfunga paka kengele? Nani atatumbua hili jipu?

Natamani waTanzania wote tulie machozi ili kuwaokoa akina Juma Kaseja, akina Nadir Haroub na akina Samatta wa miaka ijayo. Nilishasema kuwa Tanzania ni msitu mkubwa sana wa vipaji kiasi kwamba vipaji ambavyo havijakomaa tunashindwa kuvitambua maana bado tunashangaa vile vilivyokomaa. Macho yetu bado hayajachoka kuona maujanja ya Ibrahim Ajib, tunatamani kuendelea kumshuhudia Farid Mussa na bado masikio yetu yana hamu ya kusikia habari za Samatta na akina Mwaishuya. Tahamaki tahamaki 2019 imekwishafika na timu yetu ambayo ndio itakuwa mwenyeji hatujaiandaa kwa kuzikabili timu zitakazokuja. Mwaka jana wakati tangazo lile linatoka nikaona hatua za wazi zikichukuliwa na nikajua ule ni mwendo wa ku 'troti' nikaamini kuwa mwili utakapopata moto tutaanza kukimbia cha ajabu naona kama hata ku 'troti' tumeacha sasa hivi tunatembea kabisa tena mwendo wa kutoka shambani. Ukistaajabu ya Azam kuvuruga ratiba ya ligi utayaona ya U13 kusahau mipango ya kuelekea 2019.

Tumewaona Rwanda kwenye CHAN, waliyoyafanya ni macho na video ndio vitasimulia. Tumewaona Mauritius wakitupiga kule kwenye COSAFA. Tunatamani kuwafunga Algeria na Nigeria,tunatamani kuwa Spain lakini tunaizingatia jioni sana kuliko kuizingatia asubuhi yetu ya kesho. Kama tutaendelea hivi basi itatuchukua miaka zaidi ya 20 tena kumshuhudia Samatta mwingine. Hebu tutafute makabrasha ya Ghana, Mali na Germany. Ili tujue walikotoka akina Ayew, Bakayoko, Keita, Muntari na akina Gotze na Ozil. Ni kweli vipaji tunavyo vingi kiasi kwamba tunashindwa kuchagua pa kuzingatia, na ni kweli kabisa kuwa jua la mawio na machweo hufanana rangi, lakini tutazame mashariki zaidi kuliko magharibi, maana huko ndio kuna matumaini ya asubuhi.

GULINJA E. GASPER

UTAWALA WA KIHASPANIOLA KATIKA SOKA LA ULAYA

WAHISPANIA WAMETAWALA SOKA LA ULAYA.WAKATI WA KUJIULIZA Msimu uliopita Seville walitwaa ubingwa wa Ueropa league kwa kuifinga Liverpool 3-1...